ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, November 24, 2019

9 WAPOTEZA MAISHA KATIKA MAFURIKO SENGEREMA


Watu 9 wamefariki dunia  kufuatia mvua kubwa iliyonyesha wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Mvua hiyo iliyoanza kunyesha majira ya saa 12 asubuhi hadi saa 7 mchana Jumamosi ya tarehe 23 Nov 2019, licha ya vifo hivyo pia imesababisha maafa ya mafuriko yaliyo ziacha kaya kadhaa zikiwa hazina makazi, upotevu wa mali na vyakula kuharibiwa na maji.
 John Mongella ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa huo, ametia mkazo kwa kuwataka wananchi wote wanaoshi nyumba zilizo ndani au pembezoni mwa mkondo wa maji na maeneo mengine hatarishi kuhama mara moja katika kipindi hiki ambapo Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini imetoa angalizo kuwa KUTAKUWA NA VIPINDI VIFUPI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA GEITA, MARA, SINGIDA,
SHINYANGA, TABORA, SIMIYU NA MWANZA.

Akitoa taarifa ya tukio hilo kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza  John Mongella, mkuu wa wilaya ya Sengerema  Emmanuel Kipole, amesema miongoni mwa waliofariki wamo watoto watano wa kike wawili, wakiume watatu. 

Wengine wanne waliosalia watu wazima wote ni wanawake. 

  Athari na uharibifu mkubwa katika miundo mbinu ya barabara imejitokeza ikiwa ni pamoja na kukatika na kusombwa maji kwa daraja la Nyatukara lililopo katikati ya mji wa Sengerema kata ya Nyatukara mtaa wa Nyatukara.





Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.