Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limefanikiwa kuipata silaha moja aina ya bastola ikiwa na risasi tatu zinatumiwa na wahalifu (majambazi) kwenye matukio mbalimbali kanda ya ziwa baada ya watuhumiwa wawili wa ujambazi wanaume ambao bado hawajafamika majina wala makazi yao wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30, watuhumiwa hao walifariki wakati wakipelekwa hospitali baada ya majibizano ya kurushiana risasi na askari polisi baada ya kumtishia kumuua kwa bunduki na baadae kupora pikipiki ya ” mwendesha bodaboda “.
Tukio hilo limetokea tarehe 26.11.2019 majira ya 23:40hrs huko maeneo ya Sweya – Fisheries wilayani Nyamagana, hii ni baada ya mwendesha pikipiki samwel masanja (bodaboda) kuporwa pikipiki yake maeneo ya maina na watu hao na baadae wananchi kutoa taarifa polisi.
Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo askari Polisi (makachero) walifanya ufuatiliaji wa haraka na baadae wakakutana na wahalifu hao uso kwa uso maeneo ya Sweya, walipobaini kufuatiliwa walianza kuwarushia risasi askari na askari walijihami na kufanikiwa kuwajeruhi kwa risasi wahalifu hao ambao baadae walifariki dunia wakati wakipatiwa matibabu hospitali ya Bugando.
Katika eneo la tukio kumepatikana bastola moja aina ya Starbird yenye namba za usajili US Patten 2563720 pamoja na risasi tatu ndani ya magazine na pikipiki aina ya San LG nyekundu yenye namba za usajili MC 617 ABX ambayo ilikua imeporwa.
Imepatikana miili ya marehemu wote wawili imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kusubiri utambuzi na uchunguzi wa daktari.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.