ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 27, 2019

RAIS MAGUFULI MGENI RASMI MAADHIMISHO YA 58 YA UHURU WA TANGANYIKA


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Joseph Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya jamhuri zitakazofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza tarehe 9 Disemba 2019 katika viwanja vya CCM Kirumba.

Akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya wanahabari Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  John Mongella amesema kuwa sherehe hizo zinazofanyika kitaifa kwa mara ya kwanza katika Kanda ya Ziwa mkoa wa Mwanza ni za kihistoria na zitahusisha matukio mbalimbali yakiwemo Gwaride litakaloundwa na askari wa majeshi mbalimbali ya Ulinzi na Usalama nchini.

Aidha Mongella amewataka wananchi wa Mkoa wake na Kanda ya Ziwa kwa ujumla kuzichangamkia fursa mbalimbali zitakazojitokeza sanjari na kutumia maadhimisho hayo kama jukwaa la kutambulisha ustaarabu wa amani na utulivu walionao utakaotoa mwanya kuhamasisha wageni kufanya uwekezaji jijini humo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.