ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 27, 2019

CCM WAMPA ONYO BERNAD MEMBE.




Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemuonya Benard Membe, kutokuwa juu ya katiba ya chama hicho.

Onyo hilo limetolewa leo  na Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM, wakati akizungumza katika mahojiano na kipindi cha Konani kinachorushwa na Kituo cha ITV  kupitia mitandao yao ya kijamii.

Dk. Bashiru ameeleza kuwa, kama Membe ataendelea kutofuata utaratibu, uongozi wa chama hicho utamlazimisha kufuata utaratibu.

“Membe ni mwanachama mwenye haki ya kikatiba lakini ana wajibu. Kwa hiyo kama anataka kuwa mwanachama wa CCM kama walivyo wengine, lakini wametupa ushindi tunaojivunia afutae utaratibu. Asipofuata utaratibu, atalazimishwa kufuata utaratibu,” ameeleza Dk. Bashiru.

Hata hivyo, Dk. Bashiru amesema Membe hakuwahi kujadiliwa katika vikao vya chama, licha ya kwamba hakuitikia wito wake, alipomtaka kuonana nae akiwa mkoani Geita.

“Hatukuwahi kumjadili na kwenye vikao hakuwahi kufika, kosa halifi kama jinai, kosa halifi unaweza ukadhani limekufa kumbe ni utaratibu wa wakati. Kupitia kwako, naomba kueleza wana CCM tuko makini kulinda utamaduni wa chama, na wanachama kutii viapo vyao,” amesema Dk. Bashiru.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.