WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi ameendelea na mikutano yake katika Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu licha ya mvua kubwa kunyesha na kuonesha kutokata tamaa ili lengo la kuwasikiliza na kuwaeleza wananchi juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuwahudumia wafugaji.
Akizungumza na wananchi wa Mwakaluba, Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu, Waziri Mpina alisisitiza msimamo wa Serikali katika kutoa huduma bora kwa mifugo ikiwemo kupunguza gharama za uogeshaji mifugo kutoka shilingi 500 kwa kichwa cha ng'ombe hadi kufikia sh 50.
Pia Mbuzi na Kondoo kutoka shilingi 100 hadi shilingi 10 kwa kichwa cha mbuzi au kondoo hali ambayo haijawahi kutokea isipokuwa ni Serikali ya awamu ya tano pekee inayoongozwa na Rais Dk John Pombe Magufuli
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.