ZAIDI ya wanafunzi 50 wa kidato cha 1 hadi cha 4 kwa shule za sekondari katika kisiwa cha Maisome Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza wameshindwa kuendelea na masomo ya muhula wa mwaka 2018 -2019, sababu kuu zikitajwa kuwa ni mimba za utotoni, kuozwa na wazazi wao pamoja na utoro.
Hayo yamebainika kupitia ziara ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella wakati akifungua Jengo la Utawala kwa shule ya sekondari Maisome iliyopo katika kijiji cha Kisaba, kata ya Maisome wilayani humo, ambapo Shirika la Hifadhi nchini TANAPA limekabidhi nyumba ya kisasa ambapo zaidi ya shilingi milioni 100 zimegharamia ujenzi huo sanjari na thamani zilizomo ndani ya majengo.
Akionesha kusikitishwa na suala hilo Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amedhamiria kuunda kamati ya uchunguzi ili kuwabaini wahusika na kufuatilia baadhi ya kesi zilizofikishwa mahakamani.
"Hivi umeshawahi kumuona polisi akishirikiana na kibaka kuvunja nyumba?" "Ole wako mzazi uliyekula mbuzi kumuoza mwanao eti ili umalize kesi kimya kimya... Utamtapika" asema Mongella
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.