Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, ametoa msamaha kwa wafungwa 3,530 ambapo wafungwa 722 wataachiliwa huru siku ya leo April 26, 2019.
Taarifa iliyotolewa na Meja Jenerali Jacob G Kingu, imeeleza kwamba wafungwa 2808 watabaki gerezani kumalizia kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huo.
Katika kuadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Aprili 26, 2019, Rais Magufuli kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa ambapo kati ya waliopewa msamaha ni pamoja na wafungwa walioingia gerezani kabla ya machi 15, 2019.
Wafungwa wengine waliobahatika msamaha huo ni pamoja na wale wanaougua magonjwa kama Ukimwi, Kansa na Kifua kikuu ambapo watathibitishwa na Jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu Mkoa au Wilaya.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.