ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 24, 2019

BALOZI GETRUDE MONGELLA AFUNGUA TAMASHA LA 14 LA JINSIA 2019


Balozi Getrude Mongella ambaye ni Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika (PAP) na Katibu Mkuu wa Mkutano wa Nne wa wanawake duniani uliofanyika mwaka 1995 Beijing China amefungua Tamasha la 14 la Jinsia 2019 leo Jumanne Septemba 24,2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.


Akizungumza wakati wa kufungua Tamasha hilo litakalodumu kwa muda wa siku nne (Septemba 24 hadi 27,2019),Balozi Mongella maarufu 'Mama Beijing' amesema ili kujenga Tanzania ya Viwanda ni lazima wanawake na wanaume washiriki.
Balozi Mongella pia amehamasisha umuhimu wa wanawake kushirikishwa katika utengezaji wa Ilani za uchaguzi za vyama vya siasa ili kuhakikisha masuala ya wanawake yanaingizwa kufikia usawa wa kijinsia.
"Huu msemo wa Wanawake wakiwezeshwa wanaweza mimi nasema hii ni dhambi...hatupaswi kuwa omba omba...Sisi wanawake tunaweza tunachotaka ni vikwazo vinavyotukwamisha viondolewe njiani,tunataka wanawake washiriki kwenye utengenezaji wa ilani za uchaguzi ili Rais atakayegombea apewe na kubeba ajenda zinazohusu wanawake",alisema Balozi Mongella.
"Tuone masuala yanayotuhusu wanawake ni sehemu ya ajenda na uchaguzi utakapopita iwe rahisi kwa tutakayemchagua kuwa Rais kumuomba akimbizane na ajenda za wanawake na asipofanya hivyo atakuwa hajatekeleza Ilani",
Hata hivyo aliipongeza serikali kwa kutekeleza ajenda za Mkutano wa Beijing mfano Sera ya elimu bure hali inayosababisha ongezeko la watoto wa kike kwenda shule na imeondoa kikwazo cha watoto kukosa elimu.
Aidha Balozi Mongella amewataka wanasiasa kuepuka Rushwa huku akieleza kuwa Wanasiasa wanaohonga 'rushwa' ili wapate uongozi wanabaka siasa.
Naye Mgeni Maalumu kutoka serikalini,Naibu Waziri - Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alisema Ukatili wa Kijinsia ni janga jipya linaloitia doa nchi ya Tanzania hivyo kuwaomba wadau wote kuungana kutokomeza hali hiyo.
"Hatuwezi kufikia usawa wa kijinsia katika taifa kama tunaendelea kuwa na matukio ya ukatili ya kijinsia ambayo nyuma yake yana sura ya mila,desturi,umaskini na ukosefu wa elimu.Naomba tuvunje ukimya na tuepuke kumaliza kesi zinazohusu masuala ya ukatili kwa kuyamaliza kienyeje",alisema Dkt. Ndugulile.
Dkt. Ndugulile alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24,2019.
Akielezea kuhusu Tamasha la 14 la Jinsia 2019,Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi alisema linahudhuriwa na wadau mbalimbali wa haki za wanawake kutoka ndani na nje ya Tanzania likiongozwa na mada kuu 'Wanaharakati wa jinsia mbioni kubadili dunia'.
"Tamasha hili lina umuhimu wa kipekee kwani tunaendelea kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 ya TGNP tangu ianzishwe mwaka 1993 na kidunia tumeanza kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 ya Azimio na Mpangokazi wa Beijing ambapo kilele chake ni mwaka 2020",alisema Liundi.
Balozi Getrude Mongella akifungua Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam leo Jumanne Septemba 24,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Balozi Getrude Mongella akifungua Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam leo Jumanne Septemba 24,2019.
Balozi Getrude Mongella akisalimiana na Naibu Waziri - Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kufungua Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam leo Jumanne Septemba 24,2019. 
Naibu Waziri - Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Awali Balozi Getrude Mongella (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao,Asseny Muro wakifurahia jambo wakati akiwasili katika viwanja vya TGNP Mtandao kwa ajili ya kufungua Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Meza kuu wakiwa wamesimama baada ya Balozi Getrude Mongella kuwasili katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es salaam.
Washiriki wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019 wakiendelea na burudani wakati Balozi Getrude Mongella akiwasili katika viwanja vya TGNP Mtandao kwa ajili ya kufungua tamasha hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao,Asseny Muro akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
MC wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019 ambaye ni Mwanachama wa TGNP Mtandao Ulu Mallya akitoa maelekezo mbalimbali wakati wa sherehe hizo za ufunguzi wa tamasha.
Sehemu ya wageni waalikwa wakati wa tamasha hilo.
Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania,Anne Makinda akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Anders Sjoberg akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Waziri Mkuu Mstaafu Tanzania,Joseph Sinde Warioba akizungumza wakati wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Washiriki wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019 wakicheza muziki.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.