FIESTA 2014 si hii hapa...Ratiba imesha tangazwa rasmi ambapo kwa mara nyingine tena Tarehe 09 August mzigo utapigwa MWANZA. Akizungumza kupitia Clouds Fm hii leo ile mida ya XXL na B. Dozen, Mwenyekiti wa kamati ya Fiesta 2014 Sebastian Maganga amesema kuwa baada ya mikikimikiki ya shughuli mbalimbali za utafutaji na uwajibikaji kwa watanzania basi hawana budi kukutana mahali pamoja penye hadhi na service zote za uhakika kwaajili ya kupata michongo mipya huku wakitoa stress kwa kula burudani.
Mkoa wa Mwanza umepata 'shavu' kukabidhiwa funguo za burudani ya Serengeti FIESTA kwa mwaka 2014 ambapo Tarehe 09 August mzigo utapigwa pale pale palipo vunjika shoka mpini ukabakia, penye dimba lenye historia ya kuvunja rekodi ya mahudhurio CCM Kirumba MWANZA.
Maganga amesema kuwa baada ya hapo FIESTA 2014 itajisogeza ikiwa ni kwa mara ya kwanza August 15 katika mji wa BUKOBA mkoani Kagera, kisha KAHAMA 17 August nao kwa mara ya kwanza watashuhudia hizoooo shamra shamra.
Mzigo utaenda kupigwa MUSOMA 22 August, halafu vuuum SHINYANGA hii hapa tarehe 24 August. "Nafurahi kuona Shinyanga peke yake ndiyo imepewa nafasi 2 so kama utakosa Shy Town tunakutana Kahama lakini fanya tukutane zote 2 tu.... Au siyo....'Ni sheeedah!!" alisema Mwenyekiti wa kamati ya FIESTA 2014, Sebastian Maganga. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.