Taswira ya mkutano huo. |
Akizungumza na waandishi wa habari jijini
Mwanza Katibu Mkuu wa CHABATA, John Machemba alieleza maamuzi yaliofikiwa na kikao
hicho kilichofanyika hivi majuzi mkoani Shinyanga kuzungumzia mambo
mbalimbali ya mchezo huo Kanda ya Ziwa na nchi kwa ujumla.
Machemba alisema kwamba, “Tulipowaita katika kikao
baada ya kujadili tuhuma za viongozi hao wawili ili waje kujieleza kwa wajumbe
juu ya tuhuma zao ilibainika kuwa tuhuma hizo niza ukweli baada ya wao kukubali
baadhi ya tuhuma zao, hivyo kuamliwa kusimamishwa hadi kusubiri maamuzi ya
mkutano mkuu taifa,”alisisitiza.
Katibu huyo aliwataja waliosimamishwa ni Moses
Andrew (Arusha) na Lucas Bupilipili (Mwanza) ambao ni wajumbe wa Kamati hiyo
kufatia tuhuma zinazowakabili ambapo moja ya tuhuma hizo zimedaiwa ni Utovu wa
nidhamu walioonyesha hivyo kusubilia majaliwa ya maamuzi ya mkutano mkuu
utakaoketi badaye.
Naye Mwenyekiti wa Chama hicho Saimon Jackson
alieleza kuwa kikao cha kamati tendaji kiliwachagua Kamanda wa Kanda Maalum ya
Dar es salaam Seleman Kova kuendelea kuwa mlezi wa chama hicho huku Mbunge wa
zamani wa Shinyanga Leonarld Derefa akiteuliwa kuwa mshauri mkuu na wakili
Shabani Masamaki pia kuwa mshauri wa Chama hicho.
Jackson aliweka bayana gharama za mashindano ya mbio za baiskeli zilizofanyika mkoani Shinyanga zilizotolewa na wadhamini
Kampuni ya Barrick inayomiliki Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kilikuwa kiasi cha
Sh. Milioni 97.5 na kukana kuwepo matumizi mabaya ya sehemu ya fedha hizo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.