NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Mashindano ya riadha ya Transec Lake Victoria marathon kwa msimu wa tatu yanatarajia kufanyika Julai 2 mkoani Mwanza kwa kushirikisha wanariadha zaidi ya 1400 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa na maeneo mbalimbali. Hayo yamesemwa na Mratibu wa mbio hizo Halima Chake wakati wa uzinduzi uliofanyika katika uwanja wa Mwanza Yatch Club pembezoni mwa Ziwa Victoria jijini Mwanza. Chake amesema kutakuwa na mashindano ya Kilomita 2.5 kwa watoto chini ya umri wa miaka 10,kilomita 5,kilomita 10 na kilomita 2.1, huku akizitaja gharama za ushiriki kwa kiliomita ni Shilingi 20,000, Kilomita 5 ni shilingi 30,000, Kilomita 10 ni shilingi 35,000 na Kilomita 21.1 ni Shilingi 35,000. Amesema usajili umeshafunguliwa rasmi, nakutoa wito kwa wakimbiaji wote kujisajili kwa wingi tufanikishe lengo lililokusudiwa. Aidha mratibu huyo amewashukuru wadau mbali mbali kwa udhamini wao katika mbizo zao ambapo baadhi ya wadau ni Transec, benki ya KCB,TBL na Konyagi. Mnamo mwaka jana (2022) mashindano hayo yalirejesha kwa jamii kupitia kituo cha watoto wenye uhitaji kwa kuwapatia bima ya afya watoto 85. Naye Katibu Tawala msaidizi wa mkoa wa Mwanza upande wa uwekezaji na Biashara Patrick Karangwa pamoja na kuushukuru uongozi wa Lake Victoria marathon kwa kuandaa mbio hizo pia ameziomba kampuni na mashirika mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika kuunga mkono mbio hizo. Ameyataja mashindano kama chachu ya kuutangaza mkoa wa Mwanza kama sehemu ya kuhifadhi Ziwa Victoria na kuchochea biashara kwani kwenye msimu wa mbio hizi biashara zinafanyika na tukio hilo limekuwa likichochea na kukuza utalii Karangwa ameahidi kutoa ushirikiano ili kuhakikisha mbio hizo zinafanyika kwa mafanikio makubwa kama zilivyo mbio za Kilimanjaro na kwingineko. "Matukio kama haya yanawezesha kukuza uchumi, kuainsha na kuzitangaza fursa za mkoa wetu sanjari na kuwakutanisha watu kujenga uhusiano wa kibiashara huku fedha zinazochangwa zikirudi katika kuisaidia jamii. Naye ofisa Mwakilishi wa kampuni ya Transec Victor Okeyo amesema kampuni yake itaendelea kuchangia kwa kile kinachoweza kufanikisha lengo la kuisaidia jamii. "Mbio ni sehemu mojawapo ya vitu vinavyotusaidia kuwa na afya bora, nawaomba wanamichezo washiriki kwa wingi katika mbio hizi" "Kanda ya Ziwa imekuwa sehemu kubwa ya mafanikio yetu, na tunaona ni uamuzi sahihi kurudisha faida kwao" ilisema sehemu ya hotuba ya Victor Okeyo. #mwanza #samiasuluhuhassan #LakeVictoriaMarathonTupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.