NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
KIKAO cha wafanyabiashara wa bara na kumbi za starehe jijini Mwanza kimetamatika kwa maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla kuagiza #kaziiendelee kwa baa na kumbi za starehe zilizofungiwa na Baraza la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) zifunguliwe huku akipiga marufuku kamata kamata ya nguvu na kuvizia inayofanywa na baraza hilo kwa kushirikiana na jeshi la polisi.
Licha ya kuwa anakabidhiwa ofisi Mei 28 mwaka huu, Makalla ambaye aliteuliwa Mei 15 kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akitokea Dar es Salaam ametoa maagizo hayo jana Mei 26, 2023 baada ya kukutana na kusikiliza kero za wamiliki, mameneja na wafanyakazi wa baa, hoteli, kumbi za starehe na burudani jijini Mwanza. Shuhudia kikao hicho mwanzo mwisho kupitia #JembeFmTz #mwanza #samiasuluhuhassan #kaziiendeleeTupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.