Na Victor Masangu,
Jumla ya miradi 99 ya maendeleo ambayo imetembelewa na mingine kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya Asmsingi katika Mkoa wa Pwani imefanikiwa kupitishwa yote bila ya dosari yoyote na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge wakati a awwkimkabidhi rasmi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Robert Chalamila katika eneo la tazara na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama pamoja na serikali.
Kunenge alibainisha kwamba mbio za Mwenge wa uhuru ukiwa katika mkoa wa Pwani umeweza kukimbizwa umbari wa kilometa zipatazo 1201 katika Wilaya saba na halmashauri zipatazo tisa.
Alifafanua kuwa katika miradi hiyo mbali mbali ya maendeleo ambayo imeweza imegusa katika sekta mbali imegharimu jumla ya kiasi cha shilingi tilioni 4.4 ambazo zimetoka serikalini na nyingine kwa wadau wa maendeleo.
Kunenge alibainisha kuwa katika mbio hizo miradi tisa iliweza kufunguliwa na mingine 15 kuzinduliwa huku miradi mingine 20 iliweza kupata fursa ya kuwekewa mawe ya msingi huku miradi 15 imekaguliwa.
"Tunashukuru tumemaliza salama kukimbiza mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wetu wa Pwani na kwamba miradi yetu yote imeweza kupitishwa bila ya kuwa na dosari yoyote Ile kutokana na kuwa na vigezo ambavyo vinatakiwa,"alisema Kunenge.
Kwa Upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Abdalah Kaim alisema kwamba ameridhishwa na utekelezaji wa miradi mbali mbali ambayo wameweza kuitembelea.
Alimpongeza kwa dhati mkuu wa .Mkoa wa Pwani kwa kuweza kusimamia watendaji wake katika suala zima la kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo itaweza kuwasaidia wananchi.
Nao baahi ya viongozi walioudhulia katika makabidhiano hayo hawakusita kutoa pongezi kwa uongozi mzima wa Mkoa wa Pwani kwa kujitahidi kuibua miradi hiyo ambayo imefanikiwa kupitishwa yote bila kukataliwa.
Walisema kitendo cha miradi yote 99 kupitiwa na mbio za Mwenge na kufanikiwa kupitishwa bila dosari yoyote ni mafaniko makubwa kwani inaonyesha namna ya watendaji wanavyojitahidi kushirikiana bega kwa bega kwa maslahi ya wananchi kwa ujumla.
Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Pwani zimeweza kupita katika miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo kuweka mawe ya msingi.kufunguliwa,kuzinduliwa na mingine kutembelewa katika sekta tofauti.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.