ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 7, 2018

VIDEO:- MAAMUZI YA MUSUKUMA BAADA YA HABARI ZA MALI ZAKE KUPIGWA MNADA NA NBCGSENGOtV
Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku maarufu kama Musukuma amesema kuwa  waandishi wote waliomuandika kwa taarifa za uongo waombee tarehe 22 mwezi huu nyumba zake zipigwe mnada kwani isipofanyika hivyo ameapa kushughulika na mmoja baada ya mwingine.

Musukuma amesema hayo hii leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza akibu taarifa anazozitaja kuwa ni za uzushi, zilizoandikwa na moja kati ya magazeti hapa nchini, kwamba Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kupitia kampuni ya udalali ya LJ International Ltd imetangaza kuzipiga mnada mali za Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kama Musukuma.

Pia sakata hilo Mbunge Musukuma amemjumuisha Afisa wa Benki ya NBC William Kalage anayenukuliwa na gazeti hilo akithibitisha hatua za mnada huo, akimtaka amsafishe ndani ya siku 7 kabla hajachukuwa hatua za kisheria.

Mali zilizotajwa kupigwa mnada ni pamoja na kiwanja Na.275 Block kilichopo Mbezi Dar es Salaam na kiwanja Na.’2’ block ‘A’kilichopo Korogwe mjini.

Mali nyingine ni shamba Na.201 liliolopo kijiji cha Igate Mkoani Geita, kiwanja Na. 116 block A Buswelu Kaskazini na kiwanja Na. 48 block T katikati ya jiji la Mwanza.

"Hakuna nyumba yangu hata moja itakayopigwa mnada haya ni maneno ya uchonganishi, kiukweli hawatoniweza kwani siasa zangu ni za ukweli" na kisha akaongeza "Aliyeniandika ajisalimishe kabla ya tarehe aliyoitaja, kabla sijaanza kushughulika na mmoja mmoja, si mnanijua mimi ni nani........... " alimaliza Musukuma.


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya NBC, William Kalage amesema ni kweli mali hizo zinapigwa mnada.
“Ni kweli tumetoa tangazo na sisi ndiyo tumeipa kazi hiyo kampuni ya udalali kupiga mnada mali hizo,” amesema
Mbali na Musukuma, kampuni ya LJ International Ltd pia imetangaza watu 19 wanaodaiwa na benki hiyo ambao mali zao zitanadiwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.