Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ziara ya tarafa kwa tarafa ambayo anatarajia kuianza siku ya kesho katika wilaya ya Mufindi kwa lengo la kuijenga Iringa mpya yenye maendeleo
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally
Hapi anatarajia kuanza ziara ya kikazi kwa kuzitembelea tarafa zote 15 za
wilaya zote 3 za mkoa wa Iringa lengo likiwa ni kufanya jumla ya mikutano 37 na
kutembelea jumla ya miradi 55 yenye thamani ya shilingi 78,138,549,216 ambayo
itausisha ukaguzi,uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi.
Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake mh: Hapi alisema kuwa anatarajia kutembea jumla ya
kilometa 2,611 wakati wa ziara hiyo ya kikazi kwenye mkoa wote wa Iringa.
“Nitatembea tarafa tano za
wilaya ya Mufindi ambazo ni Ifwagi,Malangali,Kibengu,Sadani na Kasanga,wilaya
ya kilolo nitatembelea tarafa tatu ambazo ni Mazombe,Kilolo na Mahenge na
kumalizia wilaya ya Iringa yenye tarafa saba ambazo ni
Kalenga,Ismani,Pawaga,Idodi,Mlolo,Kiponzelo na Iringa mjini hapo ndio nitakuwa
nimemaliza ziara yangu ya tarafa kwa tarafa” alisema Hapi
Hapi alisema kuwa lengo la
ziara hiyo ni kuijenga Iringa mpya katika dhana ya kuboresha utendaji wa serikali,kuimarisha
sekta za kilimo,ujenzi wa viwanda,utalii,miundombinu,biashara,huduma za
afya,maji,elimu,utatuziwa kero za wananchi na kutengeneza fursa zilizopo katika
mkoa wa Iringa.
Aidha Hapi alisema kuwa
atafanya mikutano mikubwa kumi na saba na midogo 20 ambapo mikutano kumi na
tano itafanyika katika tarafa kumi na tano kwa kuambatana na wataalam
mbalimbali kutoka idara zote za serikali na taasisi za UMMA.
“ Katika ziara yangu zitatoa
sana fursa kwa wananchi kuuliza maswali na kutoa kero zao kwa lengo la kutatua
matatizo ambayo yanawakumba wananchi na
nitawaeleza muelekeo wa kujenga Iringa mpya” alisema Hapi
Hapi aliwataka viongozi wote wa
mkoa kuanzia wakuu wa wilaya haviongozi wa chini kuiga mfano wake wa kwenda
kutatua kero za wananchi na wasipofanya hivyo hatakuwa na msamaa kwa viongozi
wote wazembe na ambao hawatatui kero za wananchi.
Naomba kumalizia kwa kuwaomba
wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano yangu na kuhumiza viongozi
wanatakiwa kuwepo kwenye ziara yangu bila kukosa.
Believe in thomthin. Even if it meanth thacrifithing everythin
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.