ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 6, 2018

RC HAPI: MARUFUKU KUWANYANYASA MACHINGA KATIKA MAENEO WANAYOFANYIA KAZI ZAO


Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga wa manispaa ya Iringa kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto ambazo wanakabiliana katika kuleta maendeleo ya mkoa wa Iringa na kuhakikisha wanaijenga Iringa mpya ambayo inatakiwa na wanairinga 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea wakati wa kikao cha wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga na mkuu wa mkoa wa Iringa
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga walijitokeza kumsikiliza mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi na kama ambavyo unawaona walivyokuwa makini kumsikiliza hapo

 NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa mkoa wa Iringa amepiga marufuku wafanyabiashara wadogo wadogo kunyanyaswa katika mahali ambazo wanafanyia biashara kwa kuwa wanatoa kodi ambayo inachochea kuleta maendeleo ya watanzania hususani mkoani iringa tukielekea kuijenga Iringa mpya.

Akizungumza kwenye mkutano na wafanyabiasha wadogodogo wa manispaa ya Iringa mkuu wa mkoa Ally Hapi alisema kuwa wafanyabiasha wadogo wadogo maarufu kama machinga wanatakiwa kufanya biashara zao kwa kufuta taratibu na sheria za nchi huku viongozi wakiancha kuwanyanyasa kwa kuwa nao ni wafanyabiashara.

“Toka nikiwa mkuu wa wilaya najua umuhimu wafanyabiasha wadogo wadogo kwa kuchangia katika kukuza uchumi wa eneo husika hivyo natangaza rasmi ni marufuku kuwanyanyasa wafanyabiasha wadogo wadogo wa mkoa wa Iringa” alisema Hapi

Hapi aliwataka polisi wanasimamia eneo lastand kuu kuacha mara moja kunyanyasa wafanyabiasha wadogo wadogo wanaofanyia biashara katika eneo hilo.

Kauli hiyo imekuja mara baada ya katibu na mwenyekiti wa chama cha wafanyabiasha wadogo wadogo (machinga) kutoa kilio hicho mbele ya mkuu ya mkoa kwa kusema wamekuwa wakinyanyaswa na askari ambao wanafanya kazi katika stand kuu.

Katibu wa wafanyabiasha wadogo wadogo manispaa ya Iringa Joseph Kilyenyi alisema kuwa baadhi ya viongozi wa halimashauri ya manispaa ya Iringa pamoja na baadhi ya polisi wamekuwa kikwazo cha kufanya biasha kwa uhuru na kuongeza pato la manispaa ya Iringa.

“wafanyabiasha wadogo wadogo tupo zaidi ya elfu moja tukiwekewa mfumo sahihi kwa wakati sahihi tunaweza kutoa kodi zaidi ya shilingi milioni tisa  ambapo hapo tunatoa shilingi mia tatu  na ikiwa shilingi mia tano halmashauri itaingiza mapato mengi ambayo yatachangia maendeeleo ya manispaa” alisema Kilyenyi

Kilyenyi alisema kuwa wafanyabiasha wadogo wadogo wa manispaa ya Iringa wapo tayari kulipa kodi kama ambavyo Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo na kuwapa nafasi wafanyabiasha wadogo wadogo kufanya kazi kwa uhuru na kuchochoe maendeleo.

“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania DR John Pombe Magufuli amekuwa akitupelea na kuthamini hivyo hata sisi tunawajibu wa kuhakikisha tunalipa ushuru na kodi pale inapotakiwa ili kukuza juhudi za kuleta maendeleo ya nchi yetu” alisema Kilyenyi

Kilyenyi alimpongeza mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela pamoja na MNEC wa mkoa wa Iringa Salim Asas kwa kuwasaidia kutatua migogoro mbalimbali ambayo imekuwa ikiwakabili wafanyabiasha wadogo wadogo

“Baada ya kupokea kero za wafanyabiasha wadogo wadogo mkuu wa mkoa wa Iringa Hapi alimtaka Mkurugenzi wa halmashauri ya Iringa ndani ya mwezi mmoja kuhakikisha wanatengeza mfumo rafiki ambao utakuwa utasidia kukusanya kodi kwa wafanyabiasha hao.

Nimetoa siku thelathini kwa viongozi wa halmashauri kuhakikisha wanatengeza mfumo rafiki ambao hausababisha wafanyabiasha wadogo wadogo kulipa kodi katika maeneo wanayofanyia kazi ili kuwaondolea usumbufu wa kuwafuta mliko” alisema Hapi

Aidha hapi alisema kuwa hatawavumia viongozi wowote wale ambao watakwamisha kuijenga Iringa mya ambayo inatakiwa kuwa kama kituvu cha utalii nyanda za juu kusini

Naye afisa biashara wa manispaa ya Iringa kassim majariwa alisema kuwa ameyapogea maagizo yote ambayo mkuu wa mkoa ameagiza kuhakikisha kunakuwa na ongezeko la ukusanyaji wa kodi katika halmashauri ya Iringa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.