NA MWANDISHI WETU,KILINDI.
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga(NHIF) umepiga kambi Kijiji cha Gitu wilayani Kilindi mkoani humo kuhamasisha umuhimu wa mpango wa Toto Afya kadi kwa wananchi ili kuwawezesha watoto wao kupata matibabu wanapougua.
Uhamasishaji huo ulifanywa na Meneja wa Mfuko huo mkoani Tanga Ally Mwakababu akiwa ameambatana na watumishi wengine wa mfuko huo ambao walitembelea maeneo mbalimbali wilayani humo.
Akizungumza wakati akitoa elimu kuhusu umuhimu wa wananchi kujiunga na mpango huo wakiwemo watoto wao ambao utawasaidia kuweza kupata huduma za matibabu wakati wanapougua
Meneja Mwakababu alisema suala hilo ni muhimu kwa watoto wao hususani wakati wa ukuaji wao kutokana na kukabiliwa na magonjwa mbalimbali hivyo mpango huo utawasaidia wazazi kuondokana na gharama za matibabu
“Kama unavyojua huu mpango wa Toto Afya Kadi ni mzuri na unampa uhakika mtoto wako kuweza kupata huduma za matibabu pindi wanapougua kwani sio nyakati zote wanaweza kumudu gharama za matibabu kutokana na kupanda kila wakati”Alisema.
Hata hivyo aliwataka pia wananchi wa Kijiji hicho kuona namna bora ya kujiunga kwenye mfuko huo ili waweze kunufaika na huduma za matibabu wakati wanapokumbana na magonjwa mbalimbali.
Uhamasishaji huo unafanyika umefanywa na mfuko huo kwenye maeneo mbalimbali mkoani Tanga ili kuwawezesha wananchi kuchangamkia fursa hiyo wa kujiunga na mpango wa Bima ya Afya wao na Watoto wao
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.