Kufuatia kitendo hicho Rais Magufuli jana alipotembelea shule hiyo ameendelea kusisitiza kuwa viongozi waliopo serikalini aliowachagua na wale wa kuchaguliwa wachukue hatua ya kushirikiana ili kuhakikisha shule hiyo inakarabatiwa majengo yake pamoja na kujengwa uzio ili majengo ya shule hiyo kuonekena kuwa yanaubora.
"Shule aliyosoma Marehemu Mwalimu Juliujs Kambarage Nyarere mwanzilishi wa Taifa letu miaka ya 1930 inakuwa hivyo na viongozi tupo tunatakiwa kumuenzi Nyerere kwa vitendo na sio kwa maneno vawaagiza viongozi walipo serikalini kuhakikisha mnasimamia ukarabati wa shule ya Mwisenge pamoja na kujengwa uzio"alisema Magufuli.
Kauli hiyo aliitoa jana na leo kuirudia wakati alipokuwa ametembelea Mwitongo alipozaliwa Nyerere wakati akihutubia wananchi wa halmashauri ya Butiama ambapo amesema kuwa kunahaja Waziri wa Elimu kutafuta fedha mahali popote na kuhakikisha shule hiyo inakarabatiwa na kujengwa uzio na kuwa na hadhi.
"Natoa milionim20 zifanye ukarabati na wahakikishieni kuwa fedha hizo zitakuja kabla ya wiki mbili zijazo, hakikisheni haziliwi na zikafanye kazi iliyokusudiwa"
Pia Magufuli ameendelea kusema kuwa Taifa la Tanzania lazoma limuenzi Marehemu Nyerere kwasababu amehangaikia Uhuru wa Tanzania kwa kutumia juhudi zake ili kuhakikisha Tanzania inakuwa uhuru na watu wake.
Magufuli amewataka viongozi aliowachagua kuwatumikia wananchi wanyonge kwasbabu bila wananchi hao hao viongozi wasingeteuliwa kwa hali hiyo watatue matataizo ya wananchi.
Rais Magufuli baada ya kumaliza hotuba yake halmashauri ya Butiam,a alianza ziara ya kuelekea Wilaya Serengeti na kesho anatarajiwa kuingia Hlamashauri ya Tarime Vijijini na halmashauri ya Mjini wa Tarime mkoani Mara ili kusikiliza shida za wananchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.