ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 14, 2023

TRA PWANI YAWAHIMIZA WAFANYABIASHARA KUTUMIA MASHINE ZA EFD

 NA. VICTOR MASANGU,PWANI


Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani katika kupambana na kudhibiti mianya ya ulipaji wa kodi imezindua kampeni maalumu yenye lengo la kutoa elimu kwa wafanyabiashara juu kutumia mashine za kielekroniki (EFD) pindi wanapouza bidhaa zao. Hayo yamebainishwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani, Masawa Masatu wakati akizungumza na waandishi kuhusiana na kampeni hiyo ambayo pia itaenda sambamba na kuwahimiza wananchi kuhakikisha wanasai risiti pindi wanapofanya manunuzi kwani ni haki yao. Nao baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoani Pwani hawakusita kuzungumzia juu ya umuhimu wa kutumia mashine hizo za EFD huku wameipongeza TRA kwa hatua ya kwenda kuwatembea na kuwapa elimu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa maslahi ya maendeleo ya Taifa. Jisena Simon na Ramadhani Kassim Wafanyabiashara Mkoa wa Pwani. Kampeni hiyo maalumu ambayo imepewa jina la Tuwajibike itafanyika kwa kipindi cha wiki moja katika Wilaya mbalu mbali za Mkoa wa Pwani ambapo italenha zaidi kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara juu ya kutoa risiti halali pamoja na kudai risiti.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.