Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limefanikiwa kutoa elimu kwa umma ikiwa ni moja ya ya Taasisi za Kiserikali zinazoshiriki maonesho yanayoendelea katika Kongamano la Wiki ya Pili ya Ufuatiliaji (U&T).
Maonesho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya AICC jijini Arusha yalianza tarehe 12 Septemba na kilele chake ni tarehe 15 Septemba, 2023.
TASAC inashiriki maonesho hayo ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu kazi na majukumu inayoyatekeleza kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415.
Wadau wote mnaalikwa kutembelea banda la TASAC katika eneo zilipo Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Uchukuzi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.