Na Victor Masangu,Kibaha
Wananchi Wilayani Kibaha mkoani Pwani wameiomba serikali kuingilia kati changamoto ya baadhi ya askari wa maliasili kuwakamata na kuwapiga bila sababu za msingi baadhi ya watu wanaobeba mkaa kwa ajili ya matumizi yao binafsi ya nyumbani kitendo ambacho wamedai ni uonevu.
Wananchi hao wameyasema wakati wa kongamano maalumu kwa ajili ya kujadili haki jinai lililofanyika katika stendi ya zamani maili moja Wilayani Kibaha na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali taasisi binafsi,wajumbe wa tume iliyoundwa pamoja na wananchi.
Wamesema kumekuwepo na ukiukwaji wa sheria na taratibu kwa baadhi ya askari hao wa maliasili kuchukua maamuzi ambayo sio sahihi ya kuwakamata watu ambao hawana hatia na kuwachukulia mkaa kitendo ambacho wamekilaani vikali.
Kadhalika Ally Rashid ambaye ni mwananchi alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuunda time hiyo ya haki jinai ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili wananchi hasa katika kupata haki zao za msingi.
Kadhali hawakusita kutoa maoni yao juu ya adhabu kunyonga iwe pale pale na kwamba inatakiwa iundiwe kitengo chake maalumu badala ya kuacha jukumu hilo kwa Rais pekee yake na kwamba watu wanaofanya mauaji kwa makusudi adhabu hiyo iwahusu bila ya huruma.
Naye mwananchi mwingine alitejitambulisha kwa jina la Hawa John alisema kwamba kumekuwepo kwa baadhi ya polisi jamii nao wamekuwa hawatendi haki pindi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao katika kuwakamata watuhumiwa.
" Hawa polisi Jamii wako sana kwenye kata unapofika kuelezea tukio lako polisi unaambiwa uwape kwanza hela ili wakamkamate mtuhumiwa hili jambo kwetu ni kero tunaomba takukuru pamoja na Tume ilifanyie kazi"alisema
Hawa pia alisema lipo suala la baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi kutowalinda watu wanaotoa taarifa za wahalifu linapaswa kuangaliwa Ili kulinda usalama wao kwani wapo wanaopelekewa taarifa kuhusiana na wahalifu lakini haohao Askari wanawataja watoa taarifa.
Naye Ramadhani Maulidi alieleza katika mkutano huo kwamba anatamani siku moja angeajiriwa na Serikali Ili akafanye kazi ya kunyonga watu waliohukumiwa kutumikia adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na mauaji.
Alisema zipo taarifa zinazoelezwa kwenye vyombo mbalimbali kuwa ni zaidi ya miaka 10 sasa adhabu hiyo imekuwa haitekelezwi huku matukio ya mauaji yakiendelea ni wakati sasa Serikali kuliangalia suala hilo sambamba na kuajri watu wenye roho ngumu ambao watatekeleza adhabu ya kunyonga.
"Uanakuta mtu ameuwakwa makusudi halafu anaenda kukaa gerezani muda mrefu bila kunyongwa hilo haliwezekani kama mtu amekutwa na hatia ya kuuwa naye anyongwe, siyo unasikia wanaanza kusema haki za binadamu kwani yeye alipokuwa anauwa alikuwa hajui kuwa kuna haki za binadamu?" alifafanua .
Mjumbe waTume hiyo Dk Laurean Ndumbaro alisema kutosainiwa kwa adhabu ya kifo kwa watu wanaohukumiwa kutumikia adhabu hiyo kwa muda mrefu sasa kumesababisha uwepo wa mlundikano wa wafungwa na kwamba mapendekezo yao ni kuona suala hilo linangaliwa upya.
Prof. Edward Hosea ambaye ni Mjumbe wa Tume ya Haki Jinai alisema.kuwa katika ufuatiliajj wao walibaini kwamba zipo sheria nyingi zinatakiwa kufanyiwa marekebisho Ili kulinda haki za wananchi ikiwemo utitiri wa majeshi uliopo ambaounapaswa kuangaliwa na kuundiwa sheria upya.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.