Meneja wa Uwanja wa Ndege Jijini Dodoma Bertha Bankwa (wapili kulia), akimshukuru Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji (ACF) Gilbert Mvungi (watatu kulia), Kamishna Msaidizi wa Jeshi hilo ambaye ni Mkuu wa Zimamoto na Uokoaji Viwanja vya Ndege nchini (ACF) Bakari Mrisho (watatu kushoto), Kamishna Msaidizi Mstaafu wa Jeshi hilo (ACF) Christom Manyologa (kulia) kwa kuona haja ya kuandaa mafunzo hayo kwani yataongeza ufanisi katika utendaji kazi kwa Maafisa na Askari hao. Mafunzo hayo yanafanyika katika Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kiwanja cha Ndege jijini Dodoma na kuratibiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Sehemu ya Maafisa na Akari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo. Mafunzo hayo yanafanyika katika Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Ukuratibiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Kamanda
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Zimamoto na
Uokoaji (ACF) Gilbert Mvungi (watatu kulia waliokaa), Kamishna Msaidizi wa
Zimamoto na Uokoaji ambaye ni Mkuu wa Zimamoto Viwanja vya Ndege nchini (ACF)
Bakari Mrisho (watatu kushoto waliokaa), Meneja Uwanja wa Ndege Jijini Dodoma
Bertha Bankwa (wapili kulia waliokaa), Kamishna Msaidizi Mstaafu wa Jeshi hilo
(ACF) Christom Manyologa (kushoto), Mratibu wa mafunzo Uwanja wa Ndege Dodoma
Swalha Soka (wapili kushoto waliokaa), Mkuu wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji
Uwanja wa Ndege Dodoma Liberatus Monella (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja
na Maafisa na Askari wa Jeshi hilo, baada ya Kamanda wa Mkoa wa Dodoma wa Jeshi
hilo, kufungua mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo Maafisa na Akari wa
Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma.
Mafunzo
hayo yanafanyika katika Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kiwanja cha Ndege
jijini Dodoma na kuratibiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kwa
kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Aidha
imeelezwa kuwa mafunzo hayo yataendelea kwa siku tano mfululizo, na zaidi ya
Maafisa na Askari 30 watanufaika na mafunzo hayo pia yataendelea kwa Mikoa
mingine kote nchini.
Taarifa
ya Jeshi hilo imeeleza kuwa dhumuni la mafunzo hayo kuhakikisha Maafisa na
Askari wote wanaohuduma Viwanja vya Ndege kote nchini wanapatiwa mafunzo ya
aina hiyo kwa awamu hasa katika kipindi hiki tunapoelekea Tanzania ya Uchumi wa
kati unaotegemea Viwanda.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.