Dar es Salaam. Wizara ya Maji nchini Tanzania imetangaza kufuta shughuli zote zilizokua zifanyike kuelekea Siku ya Maji Duniani.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Machi 16, 2020 na Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo imesema hatua hiyo inatokana na kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona.
“Tunasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza kwa wadau wote,” ameeleza taarifa hiyo
Kufutwa kwa maadhimisho hayo, kumetolewa ikiwa ni saa chache kupita tangu Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu kutangaza raia mmoja wa nchi hiyo kubainika kuwa na ugonjwa wa Corona.
Raia huyo ambaye ni mwanamke mwenye miaka 46 aliwasili nchini humo jana Jumapili akitokea Ubelgiji.

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.