ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 16, 2020

KITUO CHA WATOTO YATIMA MSANAGANI CHAPATIWA MSAADA NA WANAWAKE WA PWANI GENERATION


 Mwenyekiti wa kikundi cha Pwani Generation  mwanamke sahihi wa kushoto akimkabidhi msaada wa vyakula mbali mbali Lilian Mbise ambaye ni Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu cha Sharom kilichopo katika eneo la Kwa mathiasi  kata ya Msangani Wilayabi Kibaha,katika halfa iliyofanyika katika kituo hicho.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

  Mlezi wa kituo cha Sharom cha kulelea watoto yatima na wale wanaosihi katika mazingira magumu Lilian Mbise wa kulia akipokea msaada wa mfuko wa mchele kutoka kwa mmoja wa wanawake wa kikundi cha Pwani Generation mwanamke sahihi wakati wa halfa fupi iliyofanyika katika kituo hicho.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Baadhi ya watoto yatima na wale amabo wanaishi katika mazingira magumu katika kituo cha Sharom kilichopo kata ya Msangani wakiimba wimbo maalumu wakati wa halfa ya kukabidhiwa msaada wa vvyakula mbali mbali kutoka na kikundi cha Pwani Generation mwanamke sahihi kwa lengo la kuwasaidia watoto hao waweze kupata mahitaji muhimu.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Mwenyekiti wa Kikundi cha PwaniGeneration Mwanamke sahihi Betty Msimbe akizungumza na watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu hawapo picha wakati wa sherehe hizo za kutoa msaada wa mahitaji mbali mbali ikiwemo vyakula.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Baadhi ya wanawake wanaounda kikundi cha Pwani Generationi mwanamke sahihi wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na yatima mara baada ya sherehe za kukabidhi vyakula mbali mbali pamoja na mahitaji mengine ya msingvi katika kituo cha Sharom kilichopo kata ya Msangani Wilayani Kibaha.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Baadhi ya wanawake wa Kikundi cha Pwani Generation mwanamke sahihi wakiwa wanawaangalia watoto hao  yatima hawapo picha pindi walipokuwa wanaimba wimbo maalumu katika halfa hiyo ya kupatiwa msaada.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Mlezi wa wa kituo cha Sharom ambacho kinalelea watoto yatima pamoja na wale amabo wanaishi katika mazingira magumu akipiga makofi kwa furaha mara baaada ya kupokea msaada huo wa vyakula mbali mbali pamoja na mahitaji mengine kutoka kwa kikundi cha Pwani Generation mwanamke(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Mlezi wa kulelea watoto yatima na wanaosihi katika mazingira magumu Lilian Mbise akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kituo hicho cha Sharaom kilipotembelewa na kikundi cha Pwani Generation mwanamke sahihi pamoja na kutoa shukrani zake za dhati kwa wanawake hao wa Mkoa wa Pwani kuweza kwenda kuwatembelea na kuwafariji (PICHA NA VICTOR MASANGU)

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha Sharom  kilichopo kata ya Msangani Wilayani Kibaha Mkoani Pwani wamemuomba Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwasaidia kwa hali na mali  kuwasaidia kuwatatulia changamoto mbali mbali zinazowakabili ikiwemo  ukosefu wa mahitaji ya chakulai,nguo, huduma za matibabu pamoja na ujenzi wa jengo la nyumba kwa ajili ya kuweza kuishi.
 Baadhi ya watoto  hao akiwemo Sara Yendemba Dickson Michael na wakizungumza wakati wa halfa ya kupokea msaada wa mahitaji mbali mbali ikiwemo chakula kutoka kwa kikundi cha Pwani Generation mwanamke sahihi walisema kwamba baada ya kuondokewa na wazazi wao wamekuwa wanaishi katika mazingira magumu  na wakati mwingine walikuwa wanakwenda kutafuta chakula majalalani hivyo wanahitaji msaada wa hali na mali kutoka serikalini na wadau wengine wa maendeleo ili waweze kujikimu kimasiha kama watoto wengine.
“Tunashukuru sana kwa msaada wa vyakula mbali mbali ambavyo tumepatiwa na  uongozi wa  wanawake wa Pwani Generation kwani utaweza kutusaidia kwani sisi hapa ni watoto yatima na wengine tunaishi katika mazingira magumu, lakini kitu kikutu bado tunamuomba Rais wetu aweze kutusaidia zaidi ujenzi wa nyumba ya kulala kwani idadi yetu ni kubwa kuliko vitanda vilivyopo”walisema watoto hao kwa masikitiko makubwa.
Pia waliongeza kwamba kabla ya kufikishwa katika kituo hicho walikuwa wanaishi mitaani kwa shida kubwa sana kutokana na kukabiliwa na changamoto mbali mbali ya kukosa mavazi, chakula sambamba na mambo mengine muhimu lakini kutokana na kituo hicho angalau wameweza kupatiwa hata fursa ya kwenda shule ya ajili ya kupata elimu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha Pwani Generation mwanamke sahihi Betty Msimbe amesema kwamba wameamua kutoa msaada huo wa mchele, mafuta, unga, sukari, pamoja na maharage katika kituo hicho kutokana na kubaini kuwepo kwa changamoto nyingi ambazo zinawakabili watoto hao ambao wanahitaji kusaidiwa mahitaji mbali mbali ili weze kujikimu kimaisha.
Mwenyekiti huyo alisema kwamba katika kikundi chao wamekuwa na utaratibu wa mara kwa mara kwenda kutoa misaada katika vituo mbali mbali vya kulelea watoto yatima na wale wanaosihi katika mazingira magumu vilivyopo katika Mkoa wa Pwani  lengo ni kuwapatia mahitaji muhimu ambayo wanastahili pamoja kwenda kuwafariji.
“Sisi kama Pwani Generation mwanamke sahihi tumeweza kubaini kuwa kituo hiki cha Sharom ambacho kipo katika Wilaya ya Kibaha bado kinakabiliwa na changamoto mbali mbali na ndio maana tukaamua kujikusanya fedha na kuamua kununua mahitaji mbali mbali ambayo wanastahili kupatiwa watoto hao kwani kutoa ni moyo na wala sio utajiri hivyo ni moja ya kuunga mkoni juhudi za serikali katika kuwasaidia watoto,”alisema Msimbe.
Naye mlezi wa Kituo hicho Lilian Mbise ambaye pia na yeye  ni yatima  amesema kwamba kituo hicho ambacho kilianzshiwa tangu mnamo mwaka 2016 kina watoto wapatao 18 ambao wanaishi katika nyumba ya kupanga hivyo kunahitajika msaada zaidi  kutoka serikalini kwa lengo la kuweza kuzitatua changamoto hizo zinazowakabili kwani mahitaji yao  ni mengi.
Kikundi hicho cha Pwani Generation mwanamke sahihi kilitoa msaada wa vitu mbali mbali mbali ikiwemo unga wa sembe, sukari, mafuta ya kula, mchele,maji pamoja na mahitaji mengine ya msingi kwa ajili ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha Sharoom ambapo vimegharimua kiasi cha zaidi ya shilingi milioni moja.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.