Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu alisema kwamba katika kutimiza azma ya Tanzania kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 serikali imedhamilia kusambaza na kuwaunganishia nishati ya umeme wa gesi asilia katika viwanda vipya vipatavyo 50 ambavyo vimepitiwa na bomba la gesi ikiwemo Mkoa wa Dar es Salaam Pwani pamoja na Mtwara na kuongeza gharama za umeme zitashuka pindi mradi wa bwawa la umeme mwalimu nyerere utakapomalika Juni 2022 na kuzalisha mega wati 2115. Mgalu ameyasema hayo wakati wa ziara ya kikazi ya kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na Madini ambayo yameifanya kwa lengo la kutembelea baadhi ya viwanda vilivyopo Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani ambavyo vinajiendesha kwa kutumia nishati ya umeme ikiwa pamoja na kuzungumza na wawekezaji ili kubaini changamoto wanazokabiliana nao na kuzitafutia ufumbuzi. Aidha Naibu Waziri huyo amebainisha kwamba kwa sasa Serikali ya awamu ya tano mpango wake mkubwa ni kuhakikisha inasambaza na kuviunganishia viwanda mbali mbali nishati ya umeme ili viweze kutimiza malengo ya azma y serikali ya kuwa na uchumi wa kati pamoja na kutoa fursa mbali mbali za ajira kwa vijana ambao ni wazalendo lengo ikiwa waweze kujikwamua na wimbi la umasikini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.