ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, August 11, 2019

SABABU YA KUPANDA BEI YA MAJI JIJINI MWANZA YAELEZWA.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA) imetoa ufafanuzi kuhusu mabadiliko mapya ya ankra za maji huku ikitumia fursa hiyo kuwaelekeza wafanyabiashara wa maji kwamba bei elekezi kwa ndoo moja ya maji yenye ujazo wa lita 20 ni shilingi 50 tu.

Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga alitoa ufafanuzi huo Agosti 09, 2019 kwenye ziara ya waandishi wa habari mkoani Mwanza kutembelea miradi mbalimbali ya maji inayosimamiwa na mamlaka hiyo ili kujifunza utendaji kazi wake.

Meza kuu:- Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga akitoa ufafanuzi kwa wanahabari (chini pichani)  kuhusu miradi ya maji inayosimamiwa na mamlaka hiyo pamoja na ongezeko la bei mpya ya maji.
Wanahabari ndani ya kusanyiko.
Yanayojiri ubaoni.

Kabla ya MWAUWASA kuwasilisha EWURA mapendekezo ya kufanya mabadiliko ya bei, ilipewa kibali na Wizara ya Maji cha kuendelea na hatua za kuwasilisha EWURA maombi ya kuongeza bei za huduma ya majisafi na usafi wa mazingira

Mara baada ya kupewa kibali na Wizara, mnamo Tarehe 15/01/2019, MWAUWASA iliitisha kikao cha Wennyeviti wa Serikali za mitaa Jijini Mwanza, Baraza la Watumiaji wa huduma za maji (EWURA CCC) na Makundi mbalimbali ya wateja wanaotumia huduma za majisafi na usafi wa mazingira. Wadau hawa walielezwa bayana nia, umuhimu na uhalisia wa kufanya mabadiliko ya bei za maji iliyolenga kuboresha huduma hiyo, ambapo wadau wote walioalikwa waliridhia na kukubaliana na mpango wa MWAUWASA kufanya mabadiliko ya bei za maji.
 Ziara imeanzia katika maabara ya Kituo cha Chanzo cha Maji Capripoint wilayani Nyamagana, jijini Mwanza.
 Wanahabari pia walitembelea mradi mpya wa maji Nyahiti wilayani Misungwi na kushuhudia kwa mara ya kwanza mashine za kusukuma maji zikiwashwa kwenye mradi huo.


Ziara hii iliratibiwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC) ikilenga pia kuimarisha mahusiano na MWAUWASA.

 Mwanahabari George Binagi akichukuwa matirio katika Kituo Cha Mradi wa Maji Nyahiti, wilayani Misungwi.
 Muonekano wa Ziwa Victoria toka chanzo cha Maji na Kituo Cha Tiba ya Maji Capripoint. 
 Eneo kubwa la jiji la Mwanza ni Mabonde na milima.

Baadhi ya Maeneo ambayo yamekuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji ambayo MWAUWASA imekusiudia kuboresha huduma hii ni pamoja na Kisesa, Bujora, Buhongwa, Kiseke, Nyasaka Islamic, Nyaaka Riverside, Ibanda, Buswelu, Nyamhongolo, Kishiri, Nyagezi Kalifonia, Ihila, Mwashi, Shadi, Biugarika, Nyakurunduma, Mabumbani, Mahina, Tambuka Reli na Maeneo mengine yaliyo kwenye miinuko Jijini Mwanza.
Wanahabari ziarani Misungwi. Hii ni taswira toka juu ya a Kituo Cha Mradi wa Maji Nyahiti, wilayani humo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.