MKUU wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ameipongeza kamati yake ya maandalizi ya maonesho ya KILIMO NANENANE 2019 kwa kufanikisha zoezi la uhamasishaji, ushiriki kwa makampuni na mashirika binafsi, sanjari na mahudhurio ya watazamaji kitendo ambacho kimeyafanya maonesho hayo kuonekana kuwa na taswira ya kipekee.
"Unapohudhuria maonesho haya na kupita kwenye mabanda mbalimbali hakikisha kuwa unatoka na kitu cha kujifunza, kitu cha kufanyia kazi katika mapinduzi yako ya maendelea hususani uwekezaji wako. Wapo wataalamu wakutosha na wawekezaji wengi wenye weredi na tija katika masuala mazima ya ujasiliamali" Mongella ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ameyasema hayo katika maadhimisho ya maonesho ya Nanenane yaliyomalizika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nyamhongolo jijini Mwanza na kupata mahudurio makubwa licha ya mikoa mingine shiriki kama Mara, Shinya na Simiyu kumegwa nao kuwa na maonesho yao .
Sanjari na hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Nane Nane 2019 katika Kanda ya Ziwa Magharibi inayohusisha mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera, Emil Kasagala ametoa taarifa ya Maonesho hayo inayoonesha mafanikio makubwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.