ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 13, 2019

KWA MARA YA KWANZA MKUU WA MKOA WA MWANZA KUPIGA KURA AKIWA MWANZA.


KWA mara ya kwanza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella atakwenda kupiga kura mkoani pake ni kupitia mabadiliko aliyoyafanya hii leo kupitia daftari la kudumu la wapiga kura.

Mapema leo asubuhi mara baada ya kuzindua rasmi zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mkoani hapa, Mongella amekuwa mtu wa kwanza kuboresha taarifa zake katika kituo cha Polisi eneo la Wazi Mtaa wa Kiseke PPF Kata ya Kiseke Manispaa ya Ilemela anakoishi.
.
.
Katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,  Mongella alipiga kura kata ya Miembeni mtaa wa Pwani Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera mahala alipojiandikishia. Hivyo hii inaashiria kua ameepuka kulazimika kusafiri hadi mjini Bukoba kwaajili ya kupiga kura 2019.
.
.
 Zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la kudumu la wapiga kura mkoani Mwanza litadumu kwa siku saba kuanzia Agosti 13-19, 2019 katika Wilaya za Ukerewe, Magu, Ilemela, Nyamagana, Sengerema na Misungwi ambapo kwa Wilaya ya Kwimba litaanza Agosti 26, 2019 hadi Septemba 01, 2019.Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.