ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 7, 2013

JAFET KASEBA NA MMALAWI KUZIPIGA

Jafet Kaseba akitunisha misuli mbele ya Anthony Ruta ambaye alikuwa akisimamia zoezi zima la upimaji akisaidiwa na ibrahim kamwe 'bigright'


KASEBA KUZIPIGA NA RASCO CHIMWANZA KESHO
 
Bondia Jafet Kaseba leo amepima tayari kumkabili mpinzani wake Rasco Chimwanza wa Malawi katika pambano la ubingwa wa kimataifa.

Zoezi zima la upimaji lilisimamiwa na Anthony ruta,ibrahim kamwe,pendo njau na doctor John Lugambila wa muhuimbili na kueleza kuwa mabondia wote wapo katika hali nzuri ya ushindani.

Kwa upande wake jafet kaseba amejinadi kumsambaratisha mpinzani wake katika raundi za mapema za mchezo huo.pia kutakuwepo na mapambano ya utangulizi kama juma fundi atazipiga na Hasan Kiwale (moro best), josef onyango toka kenya atazipiga na Seba Temba wa Morogoro,huku Issa Omar-Peche boy atakapo mvaa bondia mkongwe Juma Seleman.

Mapambano mengineyo mengi yatapigwa katika ukumbi huo wa ddc magomeni kondoa.
Nae mkongwe Juma Seleman kushoto akitunishiana misuli na bondia chipukizi kulia ISSA OMAR,hili ni moja ya pambano la kusisimua kutokana na uwezo wa wawili hao na kupaniana
 
Baadhi ya mabondia wengine watakao pigana jumamosi DDC Magomeni
Katika hali ambayo si ya kawaida kwa vyama vya ngumi hapa nchini kuwa pamoja kikazi katika mapambano wanayoyasimamia, kwa pambano la jumamosi itakuwa tofauti kwa baadhi ya maofisa wa chini wa vyama vya ngumi kusimamia mapambano kwa pamoja na kuua tofauti zao, na kujirudi kuwa wao ni wamoja katika michezo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.