Bharti Airtel yasaidia kuondoa umaskini kupitia mradi wa Millenium
Village
* Mradi huo kutoa elimu kwa wafanyakazi wa afya kwa kupitia huduma za mawasiliano
* Yawawezesha wafanyakazi 240 kuwasiliana kwa gharama nafuu za pekee.
* Airtel unasaidiana na mradi huu wa millennium village katika nchi 6 za Afrika
Dar es Salaam Juni 04 2013: Kampuni ya Bharti ("Airtel") inayoongoza kwa kutoa huduma za mawasiliano inayoendesha shughuli zake katika ndani ya nchi 20 barani Afrika na Asia, leo imethihirisha thamira yake ya kufikia malengo ya Millenium kwa kushirikiana na kampuni ya Erickson katika mradi maalum ujulikanao kama Millenum village inayoendeshwa katika nchi 6 za Afrika ikiweko Tanzania.
Mradi huo umeundwa na taasisi ya Earth Institute kwa dhamira ya kutimiza baadhi ya malengo ya Milenia kwa kuelekeza ufumbuzi wa kiubunifu zaidi katika maeneo ya vijijini huku ikishirikiana kwa ukaribu zaidi na kampuni ya simu za mkononi Airtel barani Afrika Airtel imesaidia mradi wa millennium village katika mkoa wa Tabora kwa kutoa huduma za mawasiliano zitakazowawezesha watu kupata elimu kuhusu maswala ya afya kwa urahisi. Airtel imetoa namba ya dharura itakayopigwa bila kutozwa gharama yoyote na kuwawezesha watoa huduma za afya na wagonjwa kuwasiliana kiurahisi zaidi.
Mradi wa millennium Vilage unasaidiwa na Airtel katika nchi 6 ambazo Airtel inafanya biashara zake. Nchini Tanzania mradi wa millinium village umeanzishwa katika eneo la Mbola mkoani Tabora na kusambaa katika maeneo mengi na kufikia zaidi ya vijiji 20 vilivyopo katika eneo lenye mita za mraba 700msq likiwa na wakazi 30,0000 waishio katika wilaya ya Uyui Tabora.
Mpaka sasa mradi huu umekuwa na mafanikio makubwa, zaidi ya watu 500,000 katika nchi 11 zilizoko kusini mwa jagwa la sahara Afrika wamefaidika ambapo hadi kufikia mwisho wa mwaka 2011 asiliimia 90 ya vijiji vilikuwa vimesha unganishwa na mtandao wa simu Vile vile ndani ya mradi huu kuna kipengele cha Connect to Learn, chenye ushirikiano baina ya Earth Institute Chuo kikuu cha Columbia , Ericsson and Bharti Airtel Africa, ulioanzishwa katika shule zilizopo ndani ya mradi wa millennium village na kuwafikia walimu na wanafunzi zaidi ya 5,000 katika nchi za Ghana, Tanzania, Uganda na Kenya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Bwana Sunil Colaso alisema" Airtel ina dhamira ya kugusa maisha ya watu si tu kwa kutoa huduma za mawasiliano zenye gharama nafuu lakini pia kuwazifikia jamii za chini zenye uhitaji wa technologia katika kuendeleza na kukuza maisha yao, ambayo ndio lengo lililotufanya kushirikiana na Earth Institute pamoja na Erickson kusaidia mradi huu wa millennium village.
Ushirikiano huu unatupelekea kufikia malengo ya mradi wa millennium village ya kushughulikia changamoto za umasikini katika maeneo mengi ikiwemo Kilimo, elimu, afya, miundo mbinu, usawa katika jinsia na kukua kwa Biashara. Tunafurahi kuwa sehemu ya mabadiliko na tunaahidi kuisaidia jamii nchini Tanzania.
Akiongea wakati wa halfa ya kupanua mradi wa millennium village katika kijiji cha Mbola mkoani Tabora, Meneja Huduma Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi alisema" tunafurahi kuendelea kutimiza dhamira yetu ya kutoa huduma za mawasiliano zenye gharama nafuu katika vijiji mbalimbali Tanzania .
leo tunaonyesha kwa
vitendo dhamira yetu na kuwapatia wafanyakazi 240 huduma za mawasiliano
ili kuuendesha mradi huu wa millennium village kirahisi. Airtel pia
imetoa namba ya dharura ambayo itaboresha upatikanaji wa huduma za afya ikiwemo
huduma za dharura na elimu ya afya katika kijiji cha Mbola"
"Huduma ya mawasiliano tuliyoitoa kwa wafanyakazi 240 ni pamoja na kupigiana simu kwa gharama nafuu zaidi (CUG), ujumbe mfupi wa bure pamoja na huduma ya internet ilikuwezesha mawasiliano kati yao na jamii" aliongeza Bayumi
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha huduma kwa jamii katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara Bi Margaret Kositany, alisema" ni imani yetu kwamba kwa kuboresha mawasiliano kutawezesha kuleta ufanisi katika huduma zetu za afya na kufanya mawasiliano ya karibu kati ya wauguzi na wagonjwa kuwa ya rahisi, kutoa elimu kwa jamii kupita mitandao na kuongeza uelewa wa elimu kwa njia ya mtandao kwa watoto wa shule."
"Huduma ya mawasiliano tuliyoitoa kwa wafanyakazi 240 ni pamoja na kupigiana simu kwa gharama nafuu zaidi (CUG), ujumbe mfupi wa bure pamoja na huduma ya internet ilikuwezesha mawasiliano kati yao na jamii" aliongeza Bayumi
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha huduma kwa jamii katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara Bi Margaret Kositany, alisema" ni imani yetu kwamba kwa kuboresha mawasiliano kutawezesha kuleta ufanisi katika huduma zetu za afya na kufanya mawasiliano ya karibu kati ya wauguzi na wagonjwa kuwa ya rahisi, kutoa elimu kwa jamii kupita mitandao na kuongeza uelewa wa elimu kwa njia ya mtandao kwa watoto wa shule."
Mbali na mradi wa Millennium Villages , Airtel Tanzania iko mstari wa mbele katika kusaidia shule za secondari nchini kwa kuwapati nyenzo za kufundishia ikiwemo vitabu. Tangu kuanzishwa kwa mradi wa 'Airtel Shule Yetu' zaidi ya shule 900 nchini zimefaidika na kupata vitabu kutoka Airtel.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.