ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 5, 2013

MWANZA ILIVYO ADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI HII LEO

Ujumbe wa mwaka huu juu ya siku ya mazingira.

Shughuli mbalimbali za utoaji elimu kwa wilaya za Nyamagana na Ilemela zimefanyika leo katika viwanja vya Ghand Hall jijini Mwanza.

Hili ni banda la Wizara ya maji mradi wa hifadhi ya mazingira ya ziwa Victoria (LVEMP) ambapo kulikuwa na huduma za utolewaji ufafanuzi sambamba na elimu ya utunzaji mazingira.

Hawa Abdalah ni msemaji wa banda la Wizara ya maji bonde la ziwa Victoria anasema kwamba vizibo vya soda vyaweza kutumika kutengeneza mapambo ya ndani sanjari na vibebeo kama kikapu hiki kilichodizainiwa kama mfano toka banda hili tofauti na kutupwa hovyo vikaharibu mazingira.

Muonekano zaidi.

Glory Munhambo wa banda la Bodi ya Utalii Tz mkoa wa Mwanza akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliodhuru banda lake.

Donna African Fashion (kushoto) ni moja kati ya wadau waliojitokeza kuonyesha bidhaa za nyumbani kama sehemu ya nakshi, wanapatikana Uhuru karibu na Lavena Super Market jijini Mwanza, hapa mbunifu huyu alikuwa akizungumza na mmoja ya wateja wake.

Bidhaa zizalishwazo na Donna African Fashion.

Ni bidhaa ambazo miaka ya sasa zatajwa kuvaliwa na wengi kama sehemu ya kuitikia wito  wa kuthamini bidhaa za nyumbani.

Vinogesho asili ndani ya Donna African Fashion.

Tuhamie hapa sasa.....

Mdau na wateja wake.

Dagaa na bidhaa za nafaka...

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.