Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa kwenye nyumba ya huyo mama kwa ajili ya kujiridhisha taarifa za tuhuma za kutoa mimba kwa binti wa mama huyo
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa kwenye nyumba ya huyo mama kwa ajili ya kujiridhisha taarifa za tuhuma za kutoa mimba kwa binti wa mama huyo
Na Fredy Mgunda, Iringa.
JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia Mama mmoja anayejulikana kwa jina la Egria Ngalawa kwa tuhuma za kumtoa mimba binti yake mwenye umri wa miaka 17 na kufukia kichanga Kwenye banda la kufugia nguruwe lililopo nyuma ya nyumba yao katika mtaa wa Bomba mbili kata ya Mwangata Manispaa ya Iringa.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa mtuhumiwa huyo anasadikika kutenda kosa hilo wiki moja iliyopita kwa mujibu wa taarifa alizopokea kutoka kwa raia wema.
Moyo alisema kuwa jeshi la polisi wilaya ya Iringa pia linamshikilia kwa mahojiano binti anayesadikiwa kutoa mimba hiyo na kushrikiana na mama yake kufukia kichanga hicho Kwenye banda la kufugia nguruwe.
Kiongozi huyo wa kamati ya ulinzi na usalama Iringa akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa kwa mujibu wa mahojiano Kati ya jeshi la polisi na watuhumiwa hao,inaelezwa kuwa mama wa binti huyo aliwahi kuitwa shuleni alipokuwa akisoma binti huyo nakutaalifiwa mwanae ni mjamzito.
Hata hivyo mama huyo amekana kuhusika kumtoa mimba binti yake na kufukia kichanga,akieleza kuwa Amekuwa akipokea malalamiko ya mara kwa mara ya binti yake kujihusisha kimapenzi na na wanaume za watu mtaani hapo.
Kwa upande wake binti huyo amekana kutoa mimba na kueleza kuwa hakuwahi kuwa na ujauzito wowote kwa kipindi hicho.
Aidha kulingana na maelezo hayo jeshi la polisi kwa kushirikiana na ofisi ya ustawi wa jamii limeanzisha uchunguzi wa kisayansi ili kubaini kama binti huyo anakuwa na ujauzito za siku za hivi karibuni na uchunguzi ukikamilika hatua za kisheria zitafuata.
Tukio hilo limeibuliwa ikiwa Leo ni siku ya kilele cha siku kumi na sita za kupinga ukatilii ambapo mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ametumia jukwaa la maadhimisho hayo yaliyofanyika kiwilaya katika Kijiji cha Ikuvilo kukemea vitendo vya kikatili vinavyoendelea wilaya humo huku akiwataka wananchi kupaza sauti kuwafichua watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo ili hatua za kisheria zichuliwe dhidi yao.
Moyo aliwaoonya viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji na kata kuacha tabia za kumaliza kiholela kesi za ukatilii ikiwemo ubakaji na ulawiti huku akisisitiza yeyeto atakayebainika kufanya hivyo anafunguliwa mashtaka na serikali.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.