ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, December 6, 2022

YESU HAKUTAFUTA WATU WAZURI; YESU ALITAFUTA UZURI NDANI YA WATU WABAYA

 


Yesu Hakutafuta Watu Wazuri; Yesu Alitafuta Uzuri Ndani ya Watu Wabaya: Mbinu ya 13 Aliyoitumia Kutoboa.


Denis Mpagaze

_________

Yesu alifanikiwa sana kwa sababu hiyo! Alishughulika na uzuri ulio ndani ya mtu bila kujali mtu huyo ni mzuri au mbaya maana watu wana yote; mabaya na mazuri. 


Katika hili Yesu anatufundisha kushughulika na mazuri yao, mabaya waachie wenyewe.


Sisi tunapoteza muda mwingi kutafuta watu wazuri na kuwakimbia wabaya. Utasikia ukitaka kufanikiwa katika biashara, elimu, ndoa, na ajira Find Good People! Ignore Bad People. Akina hopeless guys!


Mwisho wa siku kila mtu mzuri utakayempata utakuta ana mabaya yake yatakayokunyima hamu ya kushiriki naye katika mapenzi, biashara na kazi.🤭🤭


Unapata mume mwema, mwaminifu lakini hana hela na kumbuka kuna mambo yataendelea kuwa magumu hadi utakapopata hela.


Unapata mwenye pesa, uaminifu sifuri. Haya maisha yanavurugu nyingi!


Unapata fundi mzuri lakini mwizi wa vifaa; unapata fundi mwanifu lakini mbabaishaji.

Katika hali kama hii ni bora kufanya kazi na mtaalam mwizi unaweza kumdhibiti kuliko kufanya kazi na mbabaishaji mwaminifu!


Yesu alijua kabisa Petro atamkana lakini bado hakumny'ang'anya zile funguo za Ufalme wa mbinguni wa kufungia au kufungulia chochete (Matayo 16:13-19). 


Yesu aliona ni upuuzi kupoteza akili kubwa ya msaliti Petro kwa mambo madogomadogo. 


Yesu angekuwa Mzee Athumani, Petro angetumbuliwa siku ileile alipomkana Yesu kwa mara ya kwanza. 


Sisi kumpoteza mtu mwenye akili nyingi kwa sababu ametukosea adabu ni rahisi kama kumsukuma mlevi.


Sikiliza, ni nadra sana kumpata mtu akili na adabu kwa wakati mmoja. Kwakweli ni nadra mno. Mara nyingi watu wenye akili nyingi hawanaga adabu na wale wenye adabu sana ni zero brain. 


Nimesema ni nadra. Nadra haina maana hawapo. Wapo lakini wachache. Labda hoja hapa ni kujiuliza wewe uko kundi gani...


......inaendelea.....vipi una Sh 5,000 ya fasta nikurushie e-book ya Ukombozi wa Fikra Mpesa 0753665484!


Cheers

Mwl. Denis Mpagaze

Muhenga wa Karne ya 21!

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.