ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 8, 2014

BAR YA AR PUB WATAWAZWA KUWA MABINGWA WA SERENGETI FIESTA SOKA BONANZA 2014

Mabingwa wa Serengeti Fiesta Soka Bonanza 2014 Bar ya AR Pub toka kilimahewa jijini Mwanza akipata picha ya pamoja mara baada ya kuigalagaza Chears Pub ya Nyakato bao 1-0, mashindano yaliyofanyika katika uwanja wa Polisi Mabati jijini Mwanza.
ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA YALIYOJIRI:-
Ni mchezo wa baina ya Ar Pub na  Chears Pubbukiendelea katika uwanja wa Polisi Mabatini jijini Mwanza.
Mpira kati baada ya goli.
Pilikapilika timbwili timbwili langoni mwa Chears Pub.
Ni mwendo kusambaza upendo hapa mtangazaji wa XXL na Clouds Fm Adam Mchomvu aka Baba Jonii (mwenye miwani) alitoa fursa ya mwananchi wa 88.1 kutangaza na kuhoji wadau mbalimbali waliofika katika uwanja wa Polisi Mabatini kushuhudia Mashindano ya Serengeti Fiesta Soka Bonanza 2014..ikiwa ni shamrashamra za kuelekea Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 litakayofanyika kesho 9/08/2014 pande za CCM Kirumba Mwanza.
Mara baada ya mchezo kumalizika wananchi wakisubiri utoaji wa zawadi.
Mratibu Mkuu wa Serengeti Fiesta 2014 Shaffih Dauda akizungumzia dhima ya kuzishirikisha bar mbalimbali katika soka safari hii tofauti na ilivyozoeleka kwa kuwashirikisha mashabiki wa Vilabu vikali vinane vya soka barani ulaya, amesema kuwa nia ilikuwa ni kuwaweka karibu wadau wa mauzo na wanywaji wa Bia ya Serengeti  Lager kufahamiana na kama vipi kuweka mikakati ya kimaendeleo.
Washindi wa Serengeti Fiesta Soka Bonanza 2014 AR Pub wakishangwekaZ.
Woyooooooo......!!!

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.