Ni miaka mitano sasa tena mfululizo, klabu ya Yanga imeendelea kuwatesa watani zao Simba kwa kunyakuwa idadi kubwa ya mataji, ambapo msimu wa 2024-2025 ndiyo imekuwa kufuru zaidi, baada ya kufanikiwa kuvitia kibindoni vikombe vyote.
Mapema hii leo klabu hiyo ya Jangwani paredi la kihistoria lililo wang'aoa mashabiki wake wa viunga mbalimbali kujumika nao kila hatua walizosonga.
Katika msafara huo wa Yanga, bodaboda wamepata fursa ya kubeba mashabiki kwa kujipatia kipato, kutoka kwa mashabiki ambao wamechoka kutembea na kuamua kutumia usafiri huo.
Kutokana na msafara kuwa na magari mengi yanayotembea taratibu, kumekuwa na foleni, inayosababisha bei kuchangamka.
Pamoja na bei wanazotajiwa haionekani kuwasumbua mashabiki waliojawa na shangwe ya kusherehekea ubingwa wa msimu huu, ukiwa wa mara 31 tangu Ligi ya Bara ilipoasisiwa mwaka 1965.
Haijafahamika ni kiasi gani wanatoa kukodi usafiri huo ambao umetawaka kwenye msafara wa sherehe za ubingwa wa Yanga.
Yanga inatembeza mataji matano iliyotwaa ndani ya msimu wa 2024-2025 likiwamo Kombe la Toyota ililotwaa Afrika Kusini, Ngao ya Jamii, Kombe la Muungano, Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho ililotwaa usiku wa jana Jumapili kwa kuifunga Singida Black Stars kwa mabao 2-0.
Katika fainali hiyo ikliyopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar, mabao ya Yanga yaliwekwa kimiani na Dube Abuya na Clement Mzize na kuipa Yanga taji la nne mfululizo la michuano hiyo na la tisa kwa ujumla tangu michuano ilipoasisiwa mwaka 1967.
Tupe maoni yako



0 comments:
Post a Comment