ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 9, 2019

DHAHABU ILIYOUZWA SIKU 4 YAIZIDI ILIYOUZWA MWAKA MZIMA - SOKO LA MADINI LABAINI



SOKO jipya la Madini jijini Mwanza tayari limekwisha zinduliwa, naye Waziri wa Madini Dotto Biteko ndiye aliyesimamia hafla fupi iliyofanyika katika jengo maarufu la kibiashara Afrika Mashariki Rock City Mall ambapo tayari ametangaza kufutwa kwa kodi zilizokuwa kandamizi kwa wachimbaji wadogo na wafanyabiasha wa madini.
Akiwa na mwenyeji wake ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mwanza (John Mongella ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza) Waziri Biteko, amesema athari za faida za masoko ya madini tayari zimeanza kuonekana nchini kwani katika kipindi kifupi mathalani wilaya ya Chunya ambayo ilikuwa inaongoza kwa utoroshaji wa madini ya dhahabu ndani ya siku 4 tangu soko lake kuanzishwa imeuza Kilogram 22 ambazo hapo awali zilikuwa hazifikiwi hata kwa mauzo yake ya mwaka. Kwani hapo awali kwa mwaka, Chunya ilikuwa inauza kilogramu 12 tu ....ambazo zilikuwa zikipita katika mfumo wa uuzaji wa Serikali ........ Faida moja wapo Yya masoko hayo ya madini ni pamoja na kuzuia uuzwaji wa madini kiholela na kwa njia ya magendo, ambapo awali watu walikuwa wakichimba na kuvuna madini mbalimbali nchini Tanzania na kisha kuyakimbizia nchini za jirani kama vile Kenya ama Uganda nako ndiko walikuwa waki yaboresha katika thamani na kuyatambulisha kana kwamba yametoka kwenye nchihizo hali ambayo ilikuwa ikiishusha Tanzania kwenye takwimu za soko la madini la dunia.....

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.