Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa akiwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Robert Masunya wakati wa baraza la madiwani wakijadili kuhusu athari za wanyama Tembo na Boko
Madiwani na wataalam wa halmashauri ya wilaya ya Iringa wakiwa kwenye baraza kujadili athari zitikanazo na wanyama Tembo na Boko
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
JUMLA ya wananchi saba
wameuwawa na mnyama aina ya Boko ndani ya mwezi mmoja katika bwawa la Mtera
lililopo katika tarafa ya Ismani halmashauri ya wilaya ya Iringa huku pia
mnyama aina ya Tembo akiendelea kuharibu mazao ya wakulima wa halmashauri hiyo.
Akizungumza katika baraza la
madiwani ,diwani wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi kutoka katika
tarafa ya Ismani Yusta Kinyanga alisema kuwa mnyama aina ya Boko wamezaliana
kwa kasi kubwa na kuwa wengi katika bwawa la Mtera na kusababisha vifo vya
wananchi kutoka na wingi wao.
“Saizi Boko hao wapo wengi mno
katika bwawa hili la Mtera na kusababisha vifo vya wananchi ambavyo havina tija
yoyote na kupunguza nguvu kazi za taifa kwa kuuwawa na book hao” alisema Kinyanga
Kinyanga alisema kuwa Rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli aliagiza mamlaka
zinazohusika kuhakikisaha wanavuna Boko hao ili kupunguza vifo vya wavuvi
wanaofanya shughuli zake katika bwawa hilo.
“Alipokuwaja Rais hapa
nilimweleza juu ya swala hili la Boko na aliziagiza mamlaka husika
kushughulikia swala hilo lakini toka alipoondoka Rais hadi sasa wananchi saba
wameuuwawa kwa maana hiyo mamlaka husika zimepuuza tamko la Rais na kusababisha
vifo hivyo vya wananchi” alisema Kinyanga
Kinyanga ameiomba mamlaka
zinazohusika kuhakikisha wanawavuna Boko hao ili kupunguza vifo vya wananchi
vinavyosababisha kuacha wanawake wengi kuwa wajane kutokana na wanaume zao
kuuwa na viboko hao.
“Wanaofanya kazi ya uvuvi ni
wanaume ambao kwa asilimia kubwa wameshaoa na wanafamilia hivyo kuuwawa kwa wanaume hao kuwanawacha
wanawake kuishi bila wanaume zao hivyo kumpelekea mwanamke huyo kuwa mjane”
alisema Kinyanga
Naye diwani wa kata ya Ilolo
mpya,Fundi Mihayo amesema kuwa wanyama wa aina ya tembo wamefanya uharibifu wa
mazao wa wananchi wa kata hiyo kutokana na kuwepo kwa kundi kubwa na Tembo
ambao wanafanya uharibifu wa mazao ya wananchi.
“Mwaka huu kundi kubwa hili la
tembo hatujui limetoka wapi na limekuja kuleta athari za mazao kwa wananchi wetu na mamlaka husika hakuna
jitihada yoyote ile ambayo wanaifanya kuhakikisha wanakabiliana na tembo hao”
alisema Mihayo
Mihayo alisema athari nyingine
ambayo imejitokezani kushindwa kwa wanafunzi kwenda shuleni kwa kuhofia
kudhuliwa na Tembo ambao wamekuwa wakitembea katika maeneo hao ambao wanafunzi
hao ndio njia kuu ya kuelekea shuleni.
“Saizi wanafunzi wanaogopa hata
kwenda shule maana njia zote ambazo wanafunzi huwa wanapita kwenda shule ndio
njia ambazo kwa sasa tembo ndio maeneo ambayo wanashinda kutafuta chakula na
wameweka makazi yao” alisema Mihayo
Kwa ujumla mwaka huu hadi hivi
sasa Tembo hao wameshafanya uharibifu wa mazao katika kata ya Ilolo Mpya,Nzihi
na kata ya Kiwele na kuwaacha wananchi wasijue cha kufanya kutokana na kuwepo
kwa Tembo hao.
Kwa upande afisa maliasilia wa
halmashauri ya wilaya ya Iringa Evidence Machenje alisema kuwa serikali
imejipanga kuhakikisha wanawavuna Boko kutokana na taratibu na sheria za
wanyama pori hivyo tayarai wamewasilisha taarifa hizo kwa wizara na wanasubiri
majibu kutoka wizarani.
“Ni kweli tunataarifa za athari
zinazotokana na Boko hao hivyo sisi kama halmashauri hatuna mamlaka ya kuwavuna
wanyama hao hivyo ni lazima tuwasiliane na mamlaka husika ili waje wafanyae
utalamu wao ndipo lije swala la uvunaji wa Boko hao” alisema Machenje
Aidha Machenje amekili kuwa Tembo
na Boko wamefanya uharibifu mkubwa na kuleta madhara makubwa kwa wananchi
lakini kila kitu kinaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi hivyo
wananchi wanatakiwa kuwa na subira muda mfupi ujao kila kitu kitakuwa tayari kimefanyiwa
kazi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa, Stephen Mhapa alimwagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa matatizo hayo ya wanyama hao yanatafutiwa ufumbuzi mapema iwezekanavyo ili kuokoa maisha ya wananchi
Hata mimi ni mwadhirika kwenye kata yangu kwa Tembo kuaribu mazao ya wananchi hiki kitendo kinakera hivyo wataalam naombeni fanye haraka kuwasiliana na mamlaka husika kutatua tatizo hilo
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.