ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 9, 2019

DKT. APUMZISHWA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE



Hatimaye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited, Dkt. Reginald Mengi umezikwa katika makaburi ya familia yao yaliyopo nyumbani kwa wazazi wake, Nkuu, Machame, wilayani hai mkoani Kilimanjaro, leo Alhamisi, Mei 9, 2019.

Maelfu ya waombolezaji wamehudhuria ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi.
Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Kuu la Usharika wa Moshi mjini wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
Kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kuhudhuria ibada hiyo, polisi walilazimika kufunga barabara zote ambazo zinaelekea kwenye kanisa hilo.
Safu ya waombolezaji imeongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge la nchi hiyo Job Ndugai.

Mapema asubuhi saa tatu kanisa lilikuwa limejaa, na nje pia kulikuwa pamefurika. Baadhi ya waombolezaji walipata nafasi ya kuaga mwili ndani ya kanisa lakini ilifika mahala hatua hiyo ilisitishwa ili ibada na hotuba zitolewe.
Mwili ulitolewa kanisani kwa safari ya mwisho ya makaburini saa tisa na nusu. Na shughuli za mazishi zilikamilika saa 11 na nusu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.