SERIKALI Mkoani Mwanza Imebaini kuwepo kwa baadhi ya watendaji wa kata na mitaa ambao wameshindwa kufanya uadilifu katika zoezi la kuuza vitambusho vya wafanyabisahara wadogo vilivyotolewa na Rais Magufuli, wakidaiwa kutumia fedha za vitambulisho hivyo kwa matumizi binafsi.
Chanzo cha kubaini mchezo huo mchafu ni kufuatia taarifa za kushtua kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kushika mkia kimkoa katika mauzo ya vitambulisho kwa kukusanya asilimia 20.87 tu ya fedha, licha ya kutajwa kuwa moja kati ya wilaya zenye idadi kubwa ya wafanyabiashara hao wadogo na miundombinu ya kutosha.
Nayo Halmashauri ya wilaya ya Sengerema imeshika nafasi ya saba kwa makusanyo ya asilimia 22.52, Nafasi ya sita imeshikwa na Magu iliyokusanya asilimia 37.05, wakifuatiwa na Buchosa yenye asilimia 44.42.
Nafasi ya nne imekwenda kwa wilaya ya Ukerewe ambayo mpaka sasa imekusanya asilimia 47.88, Kwimba ni ya tatu yenye asilimia 54.28, Halmashauri ya wilaya ya Nyamagana ambayo ndiyo jiji la Mwanza imekamata nafasi ya pili kwa kukusanya asilimia 67.72, wakati Halmashauri ya wilaya ya Misungwi ikitajwa kuwa ndiyo inayoongoza kwani tayari imekusanya asilimia 80.40 za fedha za vitambulisho hivyo awamu ya pili.
Akiwa ameambatana na kamati yake ya ulinzi na usalama mkoa, John Mongella ni mkuu wa mkoa wa Mwanza na hapa anaamua kulivalia njuga suala hilo katika kikao hiki kilichofanyika kuanzia majira ya saa moja usiku na kwenda hadi usiku wa manane kikibaini baadhi ya watendaji wa halmashauri kuzifanyia matumizi mengine binafsi fedha hizo za vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo vilivyotolewa na Rais Dokta John Pombe Magufuli awamu ya pili...
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.