Liverpool ilionyesha mchezo mzuri katika historia yake baada ya kutoka nyuma na kuilaza Barcelona kwa jumla ya magoli 4-3
Baada ya kupoteza kwa magoli 3-0 katika uwanja wa Nou camp , Liverpool ililipiza kisasi wakati Divock Origi alipoiweka kifua mbele timu hiyo.
Georginio Wijnaldum alifunga magoli mawili katika dakika mbili ili kusawazisha.
Origi baadaye alifunga goli lake la pili na la nne kwa upande wa Liverpool kutokana na kona iliopigwa kwa haraka ili kukamilisha ushindi mkubwa.
Liverpooll sasa huenda ikacheza dhidi ya Ajax ama Tottenham katika fainali ya kombe la vilabu bingwa mjini Madrid mnamo tarehe mosi mwezi Juni.
Ilikuwa mazingaombwe kwa Barcelona ambao walicharazwa 3-0 na Roma katika mkondo wa pili wa robo fainali ya kombe hilo mwaka uliopita kutokana na goli la ugenini , baada ya kushinda mkondo wa kwanza 4-1.
Lakini kwa Liverpool ilikuwa kumbukumbu nyengine ya matokeo mazuri ya Ulaya ambayo yanafananishwa na ushindi wao dhidi ya AC Milan katika fainali ya 2005 na ushindi wao wa 4-3 dhidi ya Borussia Dortmund katika uwanja wa Anfield miaka mitatu iliopita.
Ni mara ya kwanza tangu 1986-wakati Barcelona ilipoilaza Gothenburg katika kombe la Ulaya-ambapo timu ilitoka nyuma kwa magoli matatu kushinda nusu fainali ya michuano hiyo.
Baada ya magoli hayo manne mashabiki wa nyumbani walisimama wakiishabikia timu yao katika dakika za mwisho huku wachezaji wa Barca walioshangazwa wakishindwa kujibu mashambulizi ya Liverpool.
Kipenga cha mwisho kilipopulizwa kilileta sherehe kubwa ndani ya uwanja na katija maeneo ya mashabiki.
Liverpool imefanikiwa kutoka nyuma na kushinda katika siku za nyuma , hususana wakati waliposhinda taji lao la tano mjini Istanbul lakini ushindi huu dhidi ya barcelona ndio mkuybwa katika historia ya klkabu hiyo wanapojiandaa kucheza dhidi katika fainali mji Madrid.
Sio mara ya kwanza kwa Barcelona kuadhibiwa kwa kiwango hiki, baada ya kufungwa 3-0 na Roma katika robo fainali mwaka uliopita baada ya kushinda mkondo wa kwanza 4-1 hivyobasi wataendelea kusubiri kutinga fainali tangu 2015.
Walichezewa katika kila safu na ijapokuwa walipata fursa kadhaa hawawezi kudai kwamba walihitaji kushinda.
Kulikuwa na kipindi kifupi katika kipindi cha kwanza , wakati mabingwa hao wa La Liga walipoamka na kuanza mchezo wao mzuri na katika kipindi cha dakika tano kipa Allison alimnyima Messi na Phillipe Coutinho huku Jordi Alba akilazimika kutoa pasi wakati ambapo alikuwa amesalia na kipa huyo kucheka na wavu.
Messi ambaye alikuwa mchezaji mwenye kasi kubwa wiki moja iliopita alishindwa kutawala hususan katika kipindi cha pili wakati magoli ya Wijnaldum yalioposawazisha.
Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez pia alipotea huku mchango wake ukionekana wakati ambapo alizomwa mara kwa mara na mashabiki ambao walizoea kumuabudu.
Alikuwa na fursa nzuri katika kipindi cha pili , wakati Messi alipompatia pasi nzuri huku Liverpool ikiwa 1-0 usiku huo lakini Allison alikuwa macho na hiyo ndio iliokuwa nafasi ya mwisho wageni hao kutekeleza tishio lolote.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.