ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 9, 2018

TCU YAISHUSHIA RUNGU CHUO HIKI, YAAMURU WANAFUNZI WAHAMISHWE.

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefuta usajili wa kituo cha chuo kikuu kishiriki cha kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo) na kuamuru wanafunzi wote wanaoendelea na masomo wahamishwe.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Novemba 9, 2018 Katibu Mtendaji wa TCU) Profesa Charles Kihampa amesema mbali ya kufuta usajili wa chuo hicho imeamuriwa pia wanafunzi wote wanaoendelea na masomo wahamishiwe katika kampasi kuu ya chuo hicho iliyopo Masoka, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Amesema TCU imezuia udahili wa wanafunzi wapya na kuamuru kuhamishwa mara moja wanafunzi wa shahada ya kwanza wanaoendelea na masomo kwa mwaka 2018/19 katika programu tisa za shahada ya kwanza  katika vyuo vikuu vinne.

Profesa Kihampa amesema wanafunzi wote wanaosoma katika chuo kikuu cha kimataifa cha tiba na teknolojia (IMTU) Dar es Salaam programu ya shahada ya tiba na upasuaji, shahada ya sayansi na uuguzi.

Amesema wanafunzi wote wanaosoma programu ya udaktari wa binadamu kutoka chuo kikuu kishiriki cha Askofu Mkuu James (Ajuco), Songea- Ruvuma.

Ametaja programu nyingine zilizozuiliwa udahili ni kutoka chuo kikuu kishiriki cha kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo) Moshi, Kilimanjaro, za shahada ya Sanaa na mawasiliano ya umma na sanaa na utawala.

Amefafanua pia imezuia udahili kwa wanafunzi wanaosoma programu za shahada ya elimu na mahitaji maalumu (arts), shahada ya elimu na mahitaji maalumu (sayansi), shahada ya sayansi na elimu na shahada ya sheria kutoka chuo kikuu cha kumbukumbu ya Sebastiano Kolowa (SEKOMU),Lushoto-Tanga.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.