ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 7, 2018

WAJANE WA AJALI YA MV NYERERE KUNUFAIKA NA BPW.


Na James Timber, Mwanza

Taasisi ya Business and Professional Women Tanzania (BPW), inatarajia kujenga kiwanda cha kutengeneza taulo za kike pamoja na kuwasaidia kwa kuwainua kiuchumi wajane wa waliopoteza wenza wao katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere kwenye Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe katika Mkoa wa Mwanza.

Akizungumza na Waadishi wa Habari jijini hapa mapema hii leo Ofisini kwake Rais wa BPW Tanzania Bertiller Massawe amesema kwa sasa wana mikakati ya kuanzisha kiwanda kwa ajili ya kutoa taulo za usafi kwa watoto wa kike hizo zitakazopatikana kwa  bei nafuu pamoja na kugawa bure kwa watoto wa shule ambao ndio waathirika wakubwa kutokana na kutokuwa na ujasiri wa kutokujiamini pamoja na kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo hasa wafikiapo siku hizo za hedhi. 

"Huu mpango tulianzisha toka Mwezi Aprili Mwaka huu na baadhi ya shule tulizofikia ni Buhongwa, Mkuyuni, Ngaza, na nyingine katika Wilaya ya Misungwi, ambapo tunaamini utumiaji mzuri wa taulo hizo zitamwezesha mwanafunzi kufanya vizuri katika masomo yake kwani atakuwa anafuatilia kimaumakini kile anachofundishwa ikiwemo uwezo wa kusimama darasani bila wasi wala hofu na kuhoji chochote na moja kati ya mikakati yetu kwa sasa iliyopo ni kufikia mwezi Januari 2019, chini ya ufadhili wa BPW kutoka nchini Italia na Malaysia tumeguswa na wanawake wajane  ambao wamekutwa na majanga tofauti ikiwemo lile na ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere," amesema.

Massawe amesema kuwa BPW inajihusisha na upimaji wa shingo ya kizazi na saratani ya matiti kwa akina mama kushirikiana na madaktari waliobobea katika taaluma hiyo, ambapo wanamwezesha mwanamke kujua hali yake kiafya kabla ugonjwa haujasambaa kwani ukiwa ugonjwa huo ukiwa sugu ni gharama kupata matibabu yake na utapekekea kudidimiza utendaji kazi wa mwanamke katika jamii.

Pia ameeleza kuwa zoezi hilo la upimaji wa shingo la kizazi na kansa ya matiti litakuwa endelevu ambapo kwa awali walitoa huduma ya upimaji kwa baadhi ya hospitali zilizopo Wilaya ya Nyamagana na Misungwi na wanatarajia kutoa huduma hiyo ya upimaji Desemba 2018, katika Chuo Kikuu cha St. Augustine SAUT  kwa wanafunzi.

Hata hivyo, mbali na upimaji wanatoa huduma ya mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi ya wananwake na vijana na kuunganishwa na taasisi ya mikopo ambayo haina riba inayotolewa na halmashauri pamoja na kuwezeshwa  kuunda vikundi vya uzalishaji mali, akiba na mikopo, ambavyo vitawapa kipaumbele kupata mikopo hiyo kwa haraka zaidi.

Aidha Rais huyo amefafanua juu ya takwimu zilizofanywa na BPW kuwa zinaonesha kuwa mabinti walioko mashuleni ni asilimia mbili ndio wanauwezo wa kutumia taulo hizo ipasavyo na wengine  kutohudhuria masomo kwa muda wa siku tatu hadi saba.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.