ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Jumla ya watumishi watano wa hospitali ya wilaya, Butimba wamesimamishwa kazi kufuatia kifo cha kichanga Novemba 3,mwaka 2018 kutokana na uzembe.
Akizungumza huku akilengwa na machozi Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Philis Nyimbi amesema kumekuwepo na malalamiko ya wananchi katika hosipitali hiyo ya Butimba kutokana na uzembe unaoneshwa na baadhi ya watumishi wa hosipitali hiyo, rushwa na kauli mbaya kwa wagonjwa wanaofika katika hosipitali hiyo kupata huduma.
Hili limejiri baada ya kutokea taarifa za kupuuzwa kwa mzazi aliyefika hospitalini hapo Jumamosi iliyopita kwa ajili ya kujifungua lakini akakosa msaada.
Watumishi waliosimamishwa kazi ni pamoja na daktari anayedaiwa kupokea pesa mkononi bila ya kutumia mfumo wa Kieletroniki wa ukusanyaji wa mapato unaotambuliwa na serikali sambamba na wauguzi wanne.
Mmoja kati ya wazazi waliokuwa wodini, Shanifa Lukas amesema licha ya hospitali hiyo kupokea wagonjwa wengi kwa siku, kuna shida kubwa kwa watumishi hususan wauguzi ambao mara nyingi wamekuwa wakitoa lugha chafu.
Tangu mwezi januari mwaka huu 2018 zaidi ya wototo wachanga wengi (TAKWIMU ZAJA) wamefariki dunia kutokana na uzembe wa baadhi ya madaktari wakati mama wajawazito wakiwa kwenye harakati za kujifungua.
Haya yanajtokeza wakati Serikali ya Tanzania ikiwa imewekeza nguvu zake katika kuimarisha mifumo ya utoaji huduma za afya ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga kwa malengo ya miaka mitano na ikiwa imekusudia kutokomeza kabisa vifo vitokanavyo na magonjwa yanayoweza kuzuilika ifikapo mwaka 2030 kama ilivyoelezwa kwenye dira ya kimataifa ya mkakati wa afya ya kila mama kila mtoto na vijana barubaru.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.