Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2019/2020 jumla ya Shilingi Bilioni 100.3
Akihitimisha hoja bungeni, Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amezungumzia suala la kampuni ya Indo-Power iliyopaswa kununua Korosho akieleza kuwa kampuni hiyo ni halali na ilikaguliwa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya.
Ameeleza kilichofanya serikali kuamua kuchana na kampuni ni kutokana na ilichelewa kutekeleza baadhi ya vipengele katika mkataba. Amesisitiza kuwa Serikali itauza korosho hivi karibuni tofauti na watu wengi wanavyofikiria
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.