ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, May 12, 2019

MKANDARASI ASAINI MKATABA MRADI WA MAJI NYASHIMO WILAYANI BUSEGA.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA) imesaini mkataba na mkandarasi kampuni ya BENNET Contractors, kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji kwa wakazi wa Kata ya Nyashimo, Wilaya Busega mkoani Simiyu.

Mkataba huo umesainiwa Mei 10, 2019 na kushuhudiwa na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka aliyebainisha kwamba kukamilika kwa miradi mbalimbali ya maji wilayani Busega, kutaongeza idadi wananchi wanaofikiwa na mtandao wa maji safi na salama kutoka asilimia 39 za sasa hadi asilimia 79.

Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga amesema utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 1.8 ni sehemu ya ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Nyashimo.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya BENNET Contractors, Sabatho Boaz ameahidi kukamilisha mradi huo kwa ubora na kwa muda wa miezi 15 kama mkataba unavyoelekeza ili kuwaondolea wananchi wa Kata ya Nyashimo adha ya upatikanaji wa maji safi na salama.
Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya BENNET Contractors, Sabatho Boaz (kulia) wakisaini mkataba wa utekelezaji mradi wa maji ya bomba katika Nyashimo wilayani Busega. Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya BENNET Contractors, Sabatho Boaz (kulia) wakibadilishana mkataba wa utekelezaji mradi wa maji ya bomba katika Kata ya Nyashimo wilayani Busega.
Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka (katikati), akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga (kushoto) baada ya kusaini mkataba wa mradi wa maji Nyashimo wilayani Simiyu. Kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya BENNET Contractors, Sabatho Boaz .
Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka akizungumza kwenye zoezi hilo la kusaini mkataba wa mradi wa maji Nyashimo wilayani Busega.
Mkuu wa Wilaya Busega, Tano Mwera amesisitiza mradi huo kukamilika kwa wakati ndani ya kipindi kilichopangwa.
Makamu Mwenyekiti Bodi ya MWAUWASA, Edith Mdogo akitoa salamu zake wakati wa zoezi la kusaini mkataba huo.
Mbunge wa Jimbo la Busega, Dk Raphael Chegeni (CCM), ameishukru Serikali kupitia Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha kutekeleza mradi wa maji Nyashimo.
Diwani wa Kata ya Nyashimo wilayani Busega, Mickness Mahela akitoa salamu zake kwenye wakati wa zoezi la kusaini mradi wa maji Nyashimo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa Mwanza, Hellen Bogoye akitoa salamu zake kwenye zoezi hilo la kusaini mradi wa maji Nyashimo wilayani Simiyu utakaosaidia kumtua mama ndoo kichwani.
Viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga (wa pili kushoto) wakiwa kwenye zoezi hilo.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Nyashimo wilayani Busega wakifuatilia zoezi hilo.
Tazama Vidio hapa chini

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.