Ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Kata ya Nyampande, Wilaya Sengerema mkoani Mwanza ya kuwaondolea adha ya upatikanaji wa maji imeanza kutekelezwa, baada ya Serikali kusaini mkataba na mkandarasi ili kutandaza mtandao wa maji ya bomba katika Kata hiyo.
Mkataba huo wa zaidi ya shilingi bilioni moja umesainiwa Mei 09, 2019 baina ya Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (MWAUWASA) pamoja na mkandarasi kampuni ya HALEM ya jijini Dar es salaam mbele ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya HALEM, Mhandisi Happy Lebe wakikabidhiana mkataba wa utekelezaji wa mradi wa maji Nyampande wilayani Sengerema baada ya pande zote mbili kuusaini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.