ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, May 12, 2019

LEO NI LEO - NANI KUTWAA TAJI LA EPL?


Bingwa wa Ligi Kuu England (EPL) kupatikana leo pale Liverpool na Manchester City watakaposhuka dimbani majira ya saa 11 jioni. 

Liverpool watacheza na Wolverhampton Wanderersm, huku Manchester City wakicheza na Brighton & Hove Albion. 

Endapo, Man City na Liverpool zote zitatoka suluhu au sare, basi Man City atakuwa bingwa. Endapo, Man City itafungwa na Liverpool kushinda, basi Liverpool watakuwa Mabingwa wa EPL na kukata kiu ya miaka 29 bila taji.

Endapo, Man City atashinda na Liverpool kushinda, maana yake Man City atakuwa Bingwa kwa tofauti ya pointi moja kama ilivyo sasa kwenye msimamo na endapo, Man City itatoa sare na Liverpool ikashinda, basi Liverpool watakuwa Mabingwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.