picha15 ikionyesha ,Rais wa chama cha wataalam waliobobea katika kupambana na ufisadi ( ACFE) ,Emanuel Johanness akiongea na waandishi wa habari
picha ikionyesha washiriki wa mkutano huo wakiendelea kufuatilia kwa makini
Na Woinde Shizza,Arusha
CHAMA cha wataalamu waliobobea katika kupambana na Ufisadi duniani (ACFE)kimejipanga kuanza kutumia teknolojia za kisasa katika kubaini na kuchunguza uhalifu huo unaoonekana kushika kazi katika nchi mbalimbali duniani.
Akiongea na waandishi wa habari leo katika mkutano mkuu wa chama hicho,unaofanyika tawi la Tanzania, jijini Arusha ,Rais wa ACFE ,Emanuel Johanness alisema lengo kubwa la mkutano huo ni kuangalia mapambano ya ufisadi katika siku za usoni kutokana na aina ya ufisadi kuhamia kwenye kiteknolojia zaidi.
Alisema taarifa yao ya mwaka jana 2018 imeonyesha kuwa katika kesi 2690 za ufisadi zilizoripotiwa kutoka nchi 125 duniani katika sekta mbalimbali 23, imeonyesha kuwa kiasi cha dolla za kimarekani billion 7 zimepotea kutokana na ufisadi unaofanyika kwenye taasisi za umma ,makampuni na sekta binafsi.
Alisema kuwa njia sahihi inayotumika kwa sasa kubaini ufisadi ni pamoja na kupewa taarifa za siri kutoka kwa wananchi wazalendo ,ambapo pamoja na mafanikio hayo ipo haja kwa chama hicho kupeana mbinu mbadala ikiwemo matumizi ya teknolojia za kisasa kubaini ufisadi.
“Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo wahalifu hawa wanavyozidi kugundua mbinu mpya za kufanya ufisadi,na ndio maana katika mkutano huu tumealika mwenzetu kutoka nchi ya Afrika kusini kuja kutupatia uzoefu wa namna wao wanavyopambana na ufisadi kwani nchi yao imefanikiwa kwa kiwango kikubwa zaidi na mapambano hayo na walianza mda mrefu kupambana na wahalifu hawa”alisemaJohaness
Akizungumzia kasi ya ufisadi hapa nchi alisema bado ni kubwa na alibainisha kuwa ufisadi mkubwa unaoongoza hapa nchi ni pamoja na rushwa,ubadhilifu wa fedha na kughushi na kwamba hatua ya serikali kuanzisha mahakama ya mafisadi itasaidia sana kupunguza uhalifu huo na kuokoa fedha za serikali kutokana na baadhi ya waalifu kukutwa na hatia na mali zao kutaifishwa .
Hata hivyo chama hicho kwa upande wa tawi la Tanzania kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kubaini matukio ya ufisadi kutokana na wanachama wake zaidi ya 200 kutoka katika sekta nyeti hapa nchini jambo ambalo limefanikisha kupata taarifa za siri na kuzifanyia uchunguzi haraka.
Kwaupande wake mmoja wa washiriki kutoka mamlaka ya mapato Tanzania TRA Salum Kessy alisema kuwa serikali ilivyoanzisha mahakama ya ufisadi ni miongoni mwa hatua nzuri kwani hata wao wanavyofanya uchunguzi ukikamilika wanapata pa kuwapeleka wahalifu hao.
Alisema kuwa iwapo watanzania tutaungana kwa pamoja zikiwemo taasisi za kiserikali pamoja na binafsi kukemea ufisadi basi tutapunguza kwa kiasi kikubwa tatizohili na sio kupunguza tu bali tunaweza kulimaliza kabisa tatizo hili.
Mkutano huo mkuu unafanyika kwa siku tatu hapa nchini na unashirikisha wataalamu kutoka nchi tano za afrika ambazo ni Kenya ,Nigeria ,Afrika kusini ,Uganda,Zambia na wenyeji Tanzania na kwamba chama hicho cha wataalamu waliobobea katika kupambana na ufisadi kina wanachama toka nchi zaidi 160 duniani na mkutano huo unatarajia kutoka na jibu moja utakaotoka na mbinu itakaomaliza ufisadi katika nchi mbalimbali duniani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.