Katika ujumbe wake wa kuthibitisha kuondoka mwisho wa msimu huu na kuwaaga mashabiki wa klabu hiyo amesema "Imekuwa miaka mitano bora, asanteni kwa kila kitu, nimewaweka moyoni mwangu."
Mchezaji huyo mwenye miaka 28 amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kwenda Barcelona tangu msimu uliopita na tetesi hizo zimeshika hatamu baada ya timu hiyo kupokea kipigo cha goli 4-0 kutoka kwa Liverpool.
Inadaiwa kuwa Barcelona ambao ni mabingwa wapya wa Ligi Kuu msimu huu nchini Uhispania, imeandaa kitita cha Paundi Milioni 108(Tsh. 321,442,041,276) ili kumsajili
Mchezaji huyo aliyejiunga Atletico mwaka 2014 akitokea Real Sociedad ameichezea timu hiyo michezo 256 na kufunga magoli 133 lakini pia amepiga pasi 50 zilizozaa magoli.
Ameiwezesha timu hiyo kushinda makombe ya Spanish Super Cup (2014-15), Europa League (2017-18) na UEFA Super Cup (2018-19).
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.