Wateja wa Airtel kulipa mikopo ya masomo kupitia huduma ya Airtel Money
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Bodi ya mikopo ya
wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) imeanzisha mapinduzi ya malipo ya
kielectoniki kwa kuwawezesha watumiaji wa huduma ya Airtel Money kulipia
mikopo ya elimu ya juu kupitia huduma ya Airtel money
Ushirikiano
huo kati ya Airtel na HESLB unawawezesha wahitimu wa masomo ya juu
katika vyuo mbalimbali nchini kuweza kulipia mikopo yao kwa urahisi
kupitia huduma ya Airtel Money na hivyo kuongeza ufanisi katika
ukusanyaji wa mikopo hiyo
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane
Matinde alisema” tumewawezesha kupitia huduma yetu ya Airtel money
wateja wetu kuweza kulipia mikopo yao ya elimu ya juu inayotolewa na
bodi ya mikopo ya elimu ya juu kirahisi wakiwa majumbani mwao.
Tunawahakikishia wateja wetu huduma bora, salama, ya uhakika yenye
viwango vya gharama nafuu na inayopatikana mahali pote nchini kupitia
mawakala zaidi ya elfu 35,000 walionea nchini.
Huduma
hii ni ya haraka na nirahisi kutumia, sasa wateja hawana haja ya
kusubiri kwenye mistari muda mrefu kufanya malipo, wanachotakiwa ni
kufanya muamala rahisi kwa kupitia simu zao kulipa na kupata
uthibithisho wa malipo ndani ya sekunde chache
Ili
kupata huduma hii mteja anatakiwa kupiga *150*60# na kuunganishwa na
orodha ya Airtel Money kasha kuchagua namba 5 kufanya malipo, alafu
chagua namba 8 kupata huduma zinginezo kisha kuandika neno HESLB ,
ingiza kiasi cha pesa, kumbukumbu namba na namba ya siri kufanya malipo
aliongeza mmbando
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu
Bwana Juma Chagonja alisema”hii imekuja wakati muafaka ambapo baadhi ya
waliofaidika na mikopo hii muda wao wa kurejesha malipo ya mikopo yao
umekwisha, kwa kupitia huduma hii ya kulipia kwa Airtel Money
hakutakuwa na haja ya watu kutembea umbali mrefu na kupanga foleni
katika mabenki ili kulipia, tunaleta kwa wateja wetu urahisi wa malipo
na njia mbadala ya kurejesha mikopo yao kwa wakati na kuongeza ufanisi
katika ukusanyaji wa mikopo hiyo.
Chagonja
aliongeza kwa kusema kwa kupitia huduma hii ya Airtel Money sasa wateja
wetu wataweza kulipa mikopo yao kirahisi wakati wowote mahali popote
masaa 24 siku 7 kwa wiki.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.